MBETO AMTAJA RAIS DKT MWINYI NI RAMANI YA MAENDELEO

 



Na Mwandishi  Wetu,Zanzibar 

CHAMA Cha Mapinduzi  kimemtaja Mgombea wake wa Urais Zanzibar Rais Dk Huseein  Ali Mwinyi  miaka mitano iliopita amekuwa dira na ramani iliofikisha Zanzibar katika  Uwanja mpana wa Maendeleo. 

Kadhalika chama  hicho , kimesifu juhudi na  utendaji wa SMZ  ,na  jina la Dk Mwinyi  limeingia  katika rekodi ya utumishi uliotukuka.

Matamshi hayo  yametamkwa na Katibu  wa Kamati  Maalum  ya NEC  Zanzibar  ,Idara ya Itikadi,Uenezi na Mafunzo ,Khamis Mbeto  Khamis  aliyesema Zanzibar  ya Mwaka 2025 kimaendeleo  si   ya Mwaka  2020.

Mbeto alisifu utendaji  wa pamoja wa SMZ  na kuitaja   miradi mikubwa  ya kisekta  ilioanzishwa na kukamilika,hivyo maendeleo  yaliopatikana yatabaki kuwa alama isiofutika .

Alisema kutokana na utendaji wa serikali ya Awamu ya Nane ,Rais Dk Mwinyi amefuata nyayo na urithi na matunda ya watangulizi wake katika kusimamia maendeleo  ya nchi na watu .

" Rais Dk  Mwinyi atabaki kuwa mfano na kielelezo cha utumishi bora. Miaka   mitano ya serikali yake ametimiza wajibu  kwa wananchi na kufanya mageuzi  makubwa katika ustawi  wa jamii " Alisema Mbeto 

Aidha, Katibu huyo Mwenezi alisema licha  ya uongozi wa Rais Dk Mwinyi kuwa kama  dira na ramani iliofikisha mbali Zanzibar kimaendeleo lakini pia wananchi waishi kwa upendo na umoja.

"Serikali  ya Awamu  ya Nane  Zanzibar  imekomesha maonevu,  ubaguzi na upendeleo. Rais  Dk Mwinyi amekataa kuongoza kwa  hasama na chuki .Serikali  yake imewajibika na kutumikia Wananchi "Alisisitiza

Pia Mbeto  alisema  hakuna jambo lolote  litakalomzuia asirudi tena ikulu,  kwani   alioyaahidi  ameyatekeleza ikiwemo kuondosha changamoto alizozikuta  na kufanikisha miradi ya kisekta.

"Wananchi  ili kumtuza Rais Dk Mwinyi wameahidi kumpigia kura nyingi ili akamilishe kazi alioianza mwaka 2020. Mgombea Urais wa CCM  hana deni kwa wananchi wake"Alisema  Katibu  huyo Mwenezi .

Comments

Popular posts from this blog

WANAFUNZI WALIOMALIZA KIDIA SEKONDARI WACHANGIA UJENZI WA KANISA SH MILLION 20

VETA YAJIPANGA KUSHIRIKINA NA TOYOTA TANZANIA KUIMARISHA MAFUNZO YA UFUNDI MAGARI

UJENZI WA BWAWA LA KUFUA UMEME LA MTO MALAGARASI , WAPIGA HATUA MPYA