MRADI WA TAZA KUFUNGUA SOKO JIPYA LA BIASHARA YA UMEME AFRIKA.

 




Wafikia asilimia 83

Dkt. Mataragio akagua mradi na kutoa maelekezo TANESCO

TAZA kuunganisha Mkoa wa Rukwa na gridi ya Taifa

Kuimarisha umeme Mikoa ya Kusini mwa Tanzania

Na Mwandishi wetu, MBEYA

IMEELEZWA kuwa mradi wa ujenzi wa njia ya kusafirisha umeme ya msongo wa kilovoti 400 kutoka Iringa hadi Zambia kupitia Tunduma (TAZA) umefikia asilimia 83.45 huku ukitarajiwa kukamilika ifikapo Mei 2026 na hivyo kufungua soko jipya la biashara ya umeme barani Afrika.

Wanafunzi wakati wa ziara ya kukagua mradi huo Oktoba 23, 2025 katika eneo la Iganjo, Mbeya, Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Nishati, Dkt. James Mataragio amesema mradi wa TAZA ni muhimu kwa Taifa kwa kuunganisha Tanzania na Nchi za ukanda wa Kusini mwa Afrika (Southern Africa Power Pool) katika mkutano wa Mashariki mwa Afrika (East Africa Power Pool).

"Nimshukuru na kumpongeza Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa fedha kwa ajili ya utekelezaji wa miradi mikubwa ya nishati. Kupitia mradi huu kufanya biashara ya kuuza na kununua umeme kati ya nchi za Mashariki mwa Afrika na zile zilizopo Kusini mwa Afrika". Amesema Dkt. Mataragio





Kuhusu biashara ya umeme ya kikanda, Dkt. Mataragio amesema kuwa tayari Tanzania imeshaunganisha gridi ya umeme na Nchi za Afrika za Kenya, Rwanda, Burundi na Ethiopia kupitia muunganiko wa East Africa Power Pool.

“Tutaunganisha pia gridi ya nchi za Kaskazini na Magharibi mwa Afrika ili Afrika nzima tuweze kuzima umeme ikiwa ni sehemu ya kutekeleza Mpango wa Nishati unaolenga kuwafikishia umeme takribani milioni 600 ambao bado hawajafikiwa na nishati ya nishati”. Amesisitiza Dkt. Mataragio.

Kuhusu mradi wa TAZA, ameeleza kuwa unatekelezwa na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa wadau wa maendeleo ambao ni Benki ya Dunia, Umoja wa Ulaya na Shirika la Maendeleo la Ufaransa kwa Dola za marekani milioni 584.

Amesema kuwa mbali ya mradi wa TAZA kuunganisha gridi ya umeme za Nchi za Kusini mwa Afrika, utaunganisha Mkoa wa Rukwa na umeme wa gridi pamoja na kuboresha hali ya umeme katika Mikoa ya Iringa, Njombe, Mbeya na Songwe.

Baada ya kukagua mradi huo, Dkt. Mataragio ameliagiza Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) kuhakikisha linamsimamia Mkandarasi kwa karibu hasa katika kipindi hiki cha mvua ili hatua za awali za ujenzi wa misingi (foundation) ziweze kukamilika kwa wakati na kumtaka Mkandarasi kuhakikisha vifaa vyote vipo eneo la Mradi.

Katika hatua nyingine Dkt. Mataragio ameiagiza TANESCO kulinda inapeleka umeme eneo la Ngozi unapotekeleza mradi eneo umeme kwa joto hivi sasa mitambo ya uhakiki wa jotoardhi katika hilo linatumia mafuta ya dizeli

Katika ziara hiyo Naibu Katibu Mkuu aliambatana na Kamishna wa Umeme na Nishati Jadidifu Mha. Innocent Luoga na watendaji wa Wizara ya Nishati na TANESCO.

Comments

Popular posts from this blog

WANAFUNZI WALIOMALIZA KIDIA SEKONDARI WACHANGIA UJENZI WA KANISA SH MILLION 20

VETA YAJIPANGA KUSHIRIKINA NA TOYOTA TANZANIA KUIMARISHA MAFUNZO YA UFUNDI MAGARI

UJENZI WA BWAWA LA KUFUA UMEME LA MTO MALAGARASI , WAPIGA HATUA MPYA