NLD, SERIKALI YA UMOJA WA KITAIFA NDIYO SULUHISHO LA TANZANIA MPYA” DOYO SINGIDA
Na Mwandishi wetu
MGOMBEA urais kupitia Chama cha NLD, Hassan Doyo, akiwa katika mkutano wa kampeni mkoani Singida, ameahidi kuwa endapo wananchi watampa ridhaa ya taifa, ataunda Serikali ya Umoja wa Kitaifa.
Amesema serikali hiyo itakuwa msingi wa kuimarisha umoja, mshikamano na maridhiano ya kitaifa, sambamba na kujenga taifa linaloongozwa kwa udilifu, uwazi na usawa.
Doyo amebainisha kuwa kupitia Serikali ya Umoja wa Kitaifa, NLD itaweza kutoa fursa kwa watu kutoka kwa ujumbe mbalimbali kushiriki moja kwa uongozi wa nchi, jambo lilitakalowezesha mawazo mapya na ubunifu katika kuliongoza taifa.
“Tunataka Tanzania yenye mshikamano katika jamii. Serikali ya Umoja wa Kitaifa itawaunganisha Watanzania wote bila kujali chama, kabila au dini kwa lengo la kuleta maendeleo ya pamoja. Nchi hii ni yetu sote, na kila mmoja anapaswa kushiriki kulijenga taifa letu kataka dhana ya kuleta maendeleo,” alisema Doyo.
Kwa mujibu wa kauli yake, serikali hiyo itakuwa chachu ya kusikiliza sauti za wananchi wote, kuondoa mpasuko wa kisiasa, na rasilimali za taifa zinatumika kwa manufaa ya wote bila upendeleo.
Aidha, Doyo ameeleza kuwa faida za Serikali ya Umoja wa Kitaifa zitahusisha kujenga mshikamano wa kitaifa kila Mtanzania atajiona sehemu ya serikali yake, migawanyiko ya kisiasa na kijamii kwa kushirikisha vyama vyote na vikundi mbalimbali, pamoja na kuwapa wananchi uwakilishi mpana imani na changamoto na mawazo yao yasikike.
Pia serikali hiyo itaimarisha amani na mshikikamo wa kitaifa, na kusema usawa katika mgawanyo wa rasilimali ili kila mkoa na kila mwananchi afaike na matunda ya taifa.
Doyo amesisitiza kuwa chama chake, NLD, kimejengwa katika misingi ya kuweka na mshikamano wa kitaifa, na nishauri atachokileta serikali mara tu baada ya kushinda uchaguzi mkuu Oktoba 29.
Katika mwendelezo wa mikutano ya kampeni, Chama cha NLD kinatarajiwa kuelekea mkoa wa Kondoa, Iringa na Njombe. @nldtanzania @tumeyauchaguzi_tanzania

Comments
Post a Comment