PURA YATOA ELIMU KWA WANANCHI KUHUSU MRADI WA UCHIMBAJI GESI RUVULA
Na Mwandishi wetu
MAMLAKA ya Udhibiti Mkondo wa Juu wa Petroli (PURA) imeeleza umuhimu wa kutoa elimu kwa wananchi kuhusu miradi inayotarajiwa kutekelezwa katika maeneo yao, ikiwa ni pamoja na uchimbaji wa visima vitatu vya asilia katika Kijiji cha Ruvula, Mtwara, kama masuala muhimu ya kuzingatia utekelezaji wa miradi hiyo kwa ufanisi.
Mjiolojia Mwandamizi kutoka kwa PURA, Ebeneza Mollel, amebainisha kuwa, pamoja na kudhibiti shughuli za kitalaamu, mamlaka inahakikisha wananchi wanapata ufahamu huo wa miradi kabla ya kuanza utekelezaji wake.
“Tunajitahidi kama mamlaka ya kusaidia jamii zinazozunguka maeneo ambayo ni mkondo wa juu wa petroli inatekelezwa zinashirikishwa katika miradi hiyo na kujengewa uelewa wa kina kuhusu mradi,” amesema Mollel.
Zoezi la kutoa elimu ya uelewa wa mradi wa uchimbaji wa visima vya gesi asilia katika Kitalu cha Mnazi Bay linafanyika katika vijiji vitatu vya Ruvula, Msimbati na Mtandi, vilivyopo katika Kata ya Msimbati, Mtwara.
Mradi huo, unaojumuisha uchimbaji wa visima viwili vya pili na kisima kimoja cha utafiti, na unatarajiwa kugharimu zaidi ya dola milioni 80.2 za Marekani, na utekelezaji wake unatarajiwa kuanza mwezi wa Desemba mwaka huu.



Comments
Post a Comment