SMZ HATA IKIJENGA BARABARA ZA DHAHABU ACT ZANZIBAR



Na Mwandishi Wetu 

CHAMA Cha Mapinduzi kimesema upinzani wa Zanzibar unachojua ni kupinga maendeleo kwasababu tu yemeletwa na SMZ hivyo hata kama zitajengwa barabara za dhahabu upinzani utapinga.

Pia CCM kimekumbusha hata Nabii Yusuf alipingwa na makuhani wa Misri , aliposhika madaraka akiwa Mtendaji Mkuu wa dola ya kifalme huko Misri .

Hayo yameelezwa na Katibu wa Kamati Maalum ya NEC ya CCM Zanzibar , Khamis Mbeto Khamis aliyesema mantiki ya kuwepo upinzani si kupinga na kubeza hata kwa mambo ya msingi. 

Mbeto alisema anashangaa kuuona upinzani hususan ACT Wazalendo , bila aibu viongozi wake wamekuwa wakiipinga juhudi za maendeleo ya kisekta yanayoonekana . 

Alisema SMZ chini ya CCM, hata ikijenga Barabara za dhababu , Majengo ya shule kwa kutumia matofali ya Almasi na lulu , ACT kitabeza na kuita huo ni mkaa wa kuni za mikarafuu .

Mbeto alikitaja kitendo cha upinzani kupinga kimaendeleo ,haukuanzishwa na ACT , kwani wapinzani wa ASP chini ya Hayati Rais Mzee Abeid Amani Karume pia walimpinga alipoleta maendeleo . 

"Maendeleo hayakuwepo Zanzibar enzi za ukoloni .Bila aibu vibaraka na wapinga maendeleo dhidi ya serikali ya ASP hawakuacha kubeza .Wapinzani wa ASP walidai SMZ haijafaanya lolote "Alisema Mbeto .

Pia Katibu huyo Mwenezi alisema hata Nabii Yusuf alipingwa na wapinzani wake asifanikishe sekta ya Kilimo cha Umwagiliaji na kujenga maghala hivyo ACT kinapopinga maendeleo ni asili ile ile ya upinzani .

'Makuhani wa Misri walimbagua Nabii Yusuf wakidai hana asili ya Misri .Wakamwita mshamba toka kijijini Canaan huko Palestina. 

Akafayiwa vituko akwane kuleta maendeleo. Alisimama imara akabadili Misri kwa muda mfupi " Alieleza 

Katibu Mwenezi huyo alisema kwa bahati nzuri , wananchi wa Zanzibar wameshapevuka kifikra na kupata mwamko hivyo wanajua kutofautisha ukweli na porojo za wanasiasa uchwara.

Comments

Popular posts from this blog

WANAFUNZI WALIOMALIZA KIDIA SEKONDARI WACHANGIA UJENZI WA KANISA SH MILLION 20

VETA YAJIPANGA KUSHIRIKINA NA TOYOTA TANZANIA KUIMARISHA MAFUNZO YA UFUNDI MAGARI

UJENZI WA BWAWA LA KUFUA UMEME LA MTO MALAGARASI , WAPIGA HATUA MPYA