USHINDI WA DEMOKRASIA SI KUACHIANA MADARAKA KIUSHEMEJI-MBETO



Na Mwandishi Wetu , Zanzibar 

CHAMA Cha Mapinduzi kimesema siku moja ikitokea CCM kimeshindwa Uchaguzi kwa matakwa ya demokrasia, hakitasita kukubali matokeo lakini hakitakiachia chama chochote utawala kwa huruma, ushemeji na hisani.

CCM kimesistiza upinzani wa Zanzibar haujapevuka na kuwa madhubuti kiasi cha kuwaridhisha wananchi ushike madaraka .

Hayo yameelezwa na Katibu wa Kamati Maalum ya NEC za Zanzibar ,Idara ya Itikadi, Uenezi na Mafunzo ,Khamisi Mbeto Khamis wakati akimjibu Mgombea Urais wa ACT Wazalendo Othman Masoud Othman. 

Mbeto alimueleza Othman kuwa wananachi bado hawakijakiamini ACT Wazalendo aidha kwa itikadi na sera zake ,misimamo yake na aina ya viongozi walionao ili kipigiwe kura za kushika utawala.

Alisema Wananchi hususan wa Zanzibar ni wakomavu kisiasa ,werevu , wanaopima mambo bila kukurupuka , hivyo hawajapata sababu ya kukiacha CCM na kuuchagua upinzani .

'Upinzani bado una kazi ya kujitafakari. Lazima wajue kwanini wananchi wanawakataa . Matamshi yao hayaonyeshi kujali umoja, viongozi wake wamejawa ubaguzi huku wengi wao wakihusishwa na tabia chafu za uhuni" Alisema Mbeto 

Aidha ,Katibu huyo Mwenezi alisema kujenga Taasisi ya kisiasa imara inayoaminiwa na wananchi, si jambo la muda mfupi, badala yake ni mchakato unayohitaji kupata sera mbadala , hoja yakinifu na dira sahihi .

"ASP toka mwaka 1957 kimevibwaga vyama vya ZNP na ZPPP. Vyama hivyo havikutokana na matakwa ya wengi . Wananchi wote waliunga mkono Sera za ASP na wagombea wake" Alikumbusha 

Mbeto alisema kizazi cha sasa kuelekea miaka hamsini ijayo,ni kile ilichotokana na Mapinduzi ya Zanzibar mwaka 1964 ambayo ndiyo yaliovunja matabaka na utawala uliodumu miaka miamoja na nne.

"Makundi ya wananachi wa kizazi hiki wamesomeshwa kwa sera za CCM .CCM kimerithi sera za TANU na ASP.SMZ imeokomesha ubaguzi,upendeleo na kuwajal wanyonge na masikini "Alieleza 

Alisema wanapotokea Wanasiasa wa upinzani na kuanza kuhubiri sera zisizoijengea matumaini jamii na kuhubiri chuki,ubaguzi na ukabila, Wananchi wana haki ya kuvikataa vyama hivyo. 

Comments

Popular posts from this blog

WANAFUNZI WALIOMALIZA KIDIA SEKONDARI WACHANGIA UJENZI WA KANISA SH MILLION 20

VETA YAJIPANGA KUSHIRIKINA NA TOYOTA TANZANIA KUIMARISHA MAFUNZO YA UFUNDI MAGARI

UJENZI WA BWAWA LA KUFUA UMEME LA MTO MALAGARASI , WAPIGA HATUA MPYA