WANAFUNZI WALIOMALIZA KIDIA SEKONDARI WACHANGIA UJENZI WA KANISA SH MILLION 20
Na Mwandishi Wetu WANAFUNZI waliomaliza kidato Cha nne mwaka 1995 katika shule ya sekondari Kidia iliyoko mkoani Kilimanjaro wamechangia zaidi ya sh mil 20 kwa ajili ya ujenzi wa Kanisa La Kiinjili La Kiluther Tanzània (KKKT) usharika Wa Kidia. Wanafunzi hao wametoa mchango huo kama shukrani na sadaka kwa Mungu kwa kuwawezesha kutumia usharika huo kwa kipindi chote walichosoma shuleni hapo lakini pia wakitumia usharika huo kwa shughuli mbalimbali ikiwemo za kielimu na kiroho pia. Mchango huo wa ujenzi pamoja na Zawadi mbalimbali ambao ni Sadaka ulikabidhiwa kanisani hapo Agosti 10,2025 katika ibada iliyoongozwa na Mkuu wa pili Wa Jimbo La Kilimanjaro Kati ambaye pia ni Mchungaji Kiongozi Usharika Wa Majengo, ,Mchungaji Israel Moshi,akishirikiana na Mchungaji Kiongozi Usharika Wa Kidia Mchungaji Sayuni Shao pamoja na Mchungaji Kiongozi Usharika Wa Kirua Mchungaji James Sambo. Akizungumza Mwenyekiti wa Umoja Wa...

Comments
Post a Comment