VIONGOZI WA DINI WAENDELEE KUHIMIZA AMANI UCHAGUZI MKUU

 




Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam

VIONGOZI wa dini nchini wameendelea kuhimiza umuhimu wa amani, umoja na uzalendo kuelekea Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 29, 2025, wakisisitiza kuwa amani ndiyo msingi wa ustawi wa taifa na halisi kwa Mungu.

Wakizungumza leo Jumatatu, Oktoba 27, 2025, katika Kongamano la Amani la Kitaifa kuelekea Uchaguzi Mkuu, lililofanyika katika Ukumbi wa Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNICC), jijini Dar es Salaam, viongozi hao wamesema jukumu la kulinda amani katika kila Mtanzania, bila kujali dini wala itikadi.

Sheikh Mkuu wa Tanzania, Dkt. Abubakar Zuberi, amesema viongozi wa dini wana wajibu wa kulinda jamii inaendelea kuwa na amani, upendo na uzalendo, hasa katika kipindi cha uchaguzi.



"Sisi kama viongozi wa dini tunalazimika kufanya kazi waliyofanya mitume kulinda amani inakuwepo ulimwenguni. Ukiwa na uzalendo utatunza amani, na kutunza amani ndiyo dini," amesema Sheikh Mkuu.

Amesema kuwa makongamano ya amani yaliyofanyika katika kanda mbalimbali za nchi yamekuwa jukwaa muhimu la kuwakumbusha Watanzania juu ya wajibu wa kulinda amani na kueleza mshikamano wa kitaifa.

Kwa upande wake, Naibu Katibu Mkuu wa Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC), Padri Chesco Msaga, amesema amani ya kweli huanzia ndani ya moyo wa mtu binafsi kabla ya kuonekana katika jamii.

“Amani ya kweli inaanzia ndani ya roho Kama sina amani moyoni siwezi nikapeleka amani kwa mtu mwingine,” amesema.

Mkurugenzi wa Al Hikma Foundation, Sheikh Nurdin Kishki, amewataka Watanzania kuendelea kulitetea taifa kwa maneno na matendo ya kizalendo, akisema ni kosa kwa mtu kutaka kuvuruga amani kwa kisingizio cha maoni binafsi.

“Siku hizi ukisimama kulitetea taifa lako unaambiwa umepewa bahasha. Lakini nataka kuuliza, wale wanaotaka kuvunja amani wanapewa na nani?” amehoji.

Naye Mwenyekiti wa Jumuiya ya Makanisa ya Tanzania (JMAT-TAIFA), Alhad Mussa Salum, ametoa wito kwa wazazi na viongozi kuwaelimisha vijana, hasa wa kizazi cha Gen Z, juu ya thamani ya nchi na madhara ya vurugu.


"Changamoto hazitatuliki kwa utaratibu bali kwa utaratibu. Tuwasihi wetu kwamba kuiharibu na kisha kuitengeneza upya si jambo la busara," amesema.

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Makanisa ya Kipentekosti Tanzania (CPCT), Dk. Vernon Fernandes, amesema na mafanikio yaliyopo nchini hayawezi kudumu bila uwepo wa amani, akiwa amejitokeza kupiga kura ili kupokea.

Wakati huo huo, Serikali imetoa shukrani kwa viongozi wa dini kupitia Kamati ya Amani kwa juhudi zao za kulipwa na mshikamano wa kitaifa.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Mipango na Uwekezaji), Prof. Kitila Mkumbo, aliyemwakilisha Makamu wa Rais, Dk. Philip Mpango, wakati wa kufunga kongamano hilo, amesema makongamano ya amani yamekuwa chachu ya kuimarisha imani ya wananchi kuelekea uchaguzi.

“Tafiti zinaonyesha wananchi wengi wanawaamini zaidi viongozi wa wanapokuwa kwenye changamoto zao. Kwa mchango wenu ni mkubwa sana katika kulinda Watanzania wanashiriki uchaguzi kwa amani,” amesema Prof. Mkumbo.

Ameongeza kuwa huu ni uchaguzi wa 14 tangu Tanzania ianze mfumo wa vyama vingi, hivyo ni kipindi muhimu zaidi kuhusu amani kama urithi wa taifa.

Kongamano hilo limehitimisha mfululizo wa makongamano ya amani yaliyofanyika nchini kupitia kanda zote Kusini, Kaskazini, Kati, Magharibi na Nyanda za Juu Kusini zilitibiwa na Kamati ya Amani ya Kitaifa.



Comments

Popular posts from this blog

WANAFUNZI WALIOMALIZA KIDIA SEKONDARI WACHANGIA UJENZI WA KANISA SH MILLION 20

VETA YAJIPANGA KUSHIRIKINA NA TOYOTA TANZANIA KUIMARISHA MAFUNZO YA UFUNDI MAGARI

UJENZI WA BWAWA LA KUFUA UMEME LA MTO MALAGARASI , WAPIGA HATUA MPYA