AJIRA 12,000 KUWANUFAISHA VIJANA WA TANZANIA
Na Mwandishi wetu
WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. Ridhiwani Kikwete ameitaka Sekreterieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma kuharakisha na kuweka wazi mchakato wa Ajira 12,000 zilizotangazwa hivi karibuni na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan wakati akifungua Bunge la 13 Novemba 14, 2025 Jijini Dodoma.
"Moja ya ahadi za Rais Samia ni kuhakikisha utumishi wa umma unakua bora katika kutoa huduma kwa wananchi na ndiyo maana akatoa kibali cha Ajira 12,000 kwa kada ya Elimu Ajira 7,000 na Afya Ajira 5,000".
"Tuongeze kasi ya kuratibu utoaji wa Ajira hizi, kibali kimeshatolewa, nawashukuru kwa kuanza kufanyia kazi lakini hakikisheni mnasimamia kikamilifu, mchakato wote wa Ajira hizi uwekwe wazi ili kuondoa dhana potofu ya upendeleo. Tuzingatie maadili ili kuhakikisha wanapatikana watumishi sahihi na wenye vigezo." Alisema Kikwete.
Aidha, Waziri Kikwete amesisitiza Sekreterieti hiyo ya Ajira kutoonea watumishi walio chini yao bali wawaelekeze kwa upendo


Comments
Post a Comment