WAZIRI NDEJEMBI AWATAKA PBPA KUHAKIKISHA KUNAKUWEPO NA AKIBA YA KUTOSHA YA MAFUTA NCHINI



Ahimiza uboreshaji wa Miundombinu ya kupokelea mafuta

Ahimiza kutokuwepo na ucheleweshaji kwenye uingiaji wa mafuta nchini.

Alekeza ushirikishwaji wa Wadau katika  kuwekeza kwenye ujenzi wa miundombinu ya kuhifadhia mafuta


Na Mwandishi wetu

WAZIRI wa Nishati Deogratius Ndejembi amewataka Wakala wa Kuagiza Mafuta kwa Pamoja( PBPA) kuhakikisha kunakuwepo na akiba ya kutosha ya mafuta nchini lengo likiwa ni kuhakikisha uendelevu wa  shughuli za uzalishaji, usafirishaji na huduma nyingine muhimu ambazo zinategemea kwa kiasi kikubwa nishati hiyo 

Ndejembi ameyasema hayo Novemba 25,2025 Jijini Dar es salaam katika ofisi za PBPA ikiwa nimuendelezo wa ziara yake ya kuzungumza na viongozi wa Taasisi zilizoko chini ya Wizara ya Nishati

Ametoa maelekezo kwa PBPA  kuhakikisha akiba ya mafuta hapa nchini inakuwa ya kutosha kwani itasaidia kuepuka uhaba wa ghafla unaoweza kusababisha ongezeko la gharama kwa wananchi na sekta binafsi na kukosekana kwa huduma hiyo.



“Akiba ya mafuta ya kutosha kupitia uwekezaji katika vituo vya kuhifadhi kunaleta utulivu wa kiuchumi kwa Taifa kwani kunapokuwa na uhakika wa upatikanaji wa mafuta, shughuli za uzalishaji, usafirishaji na biashara zinaendelea bila vizuizi na hii huongeza imani ya wawekezaji, hupunguza gharama za dharura, na hatimaye  kukuza ukuaji endelevu wa uchumi”.Amesisitiza Mhe. Ndejembi

Aidha Ndejembi amewataka viongozi wa PBPA kuhakikisha wanawekeza zaidi katika kuimarisha miundombinu ya kupokelea mafuta  na kuhifadhia mafuta ili kuboresha usalama na ubora wa bidhaa kwa maslahi mapana ya Taifa 

Sambamba na hilo  Ndejembi amesisitiza wakala hao kushirikiana na wadau wa sekta binafsi kwenye mnyororo wa usambazaji mafuta lengo likiwa ni kuhakikisha upatikanaji wa maghala ya kuhifadhia mafuta ili kuondoa ucheleweshaji wa mafuta au upungufu usiotarajiwa.




 Awali akiwasilisha taarifa  ya utendaji kazi Afisa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa kuagiza mafuta kwa pamoja   Erasto Simon ameeleza kuwa Katika kuhakikisha ufanisi katika utendaji kazi PBPA imejiandaa kuunganisha mifumo itakayosaidia kutoa bei linganifu kwenye bandari zote ili kuleta ufanisi katika usambazaji wa mafuta.

Katika ziara hiyo,  Ndejembi ameambatana na Katibu Mkuu Wizara ya Nishati, Mhandisi Felchesmi Mramba pamoja na watalaamu wengine wa wizara.




Comments

Popular posts from this blog

WANAFUNZI WALIOMALIZA KIDIA SEKONDARI WACHANGIA UJENZI WA KANISA SH MILLION 20

VETA YAJIPANGA KUSHIRIKINA NA TOYOTA TANZANIA KUIMARISHA MAFUNZO YA UFUNDI MAGARI

UJENZI WA BWAWA LA KUFUA UMEME LA MTO MALAGARASI , WAPIGA HATUA MPYA