DKT. MWIGULU AKAGUA UHARIBIFU WA KITUO CHA POLISI KIKATITI

 


WAZIRI Mkuu  Dkt. Mwigulu Nchemba, leo Novemba 30, 2025, amekagua Kituo cha Polisi Kikatiti ambacho kiliharibiwa kutokana na vurugu zilizotokea Oktoba 29, 2025, mkoani Arusha.

Akizungumza na wakazi wa eneo hilo, Dkt. Mwigulu amewataka wananchi kuwa makini dhidi ya watu wasiolitakia mema Taifa kwa kuchochea vurugu na kuharibu miundombinu ya umma na ya binafsi.

Dkt. Mwigulu yupo mkoani Arusha kwa ziara ya kukagua uharibifu uliojitokeza kufuatia vurugu za Oktoba 29, 2025.




Katika ziara hiyo,  Dkt. Mwigulu ameambatana na Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Amosi Makalla.




Comments

Popular posts from this blog

WANAFUNZI WALIOMALIZA KIDIA SEKONDARI WACHANGIA UJENZI WA KANISA SH MILLION 20

VETA YAJIPANGA KUSHIRIKINA NA TOYOTA TANZANIA KUIMARISHA MAFUNZO YA UFUNDI MAGARI

UJENZI WA BWAWA LA KUFUA UMEME LA MTO MALAGARASI , WAPIGA HATUA MPYA