MBUNGE MAVUNDE AANZISHA UJENZI WA ZAHANATI MTAA WA MASEYA-HOMBOLO MAKULU






Wananchi wanampongeza kwa kutimiza ahadi yake

Aapa ujenzi kwa wakati

Wananchi wamshukuru Rais Samia kwa visima vya umwagiliaji na Umeme

Na Mwandishi wetu

MBUNGE wa Jimbo la Mtumba Mh. Anthony Mavunde leo ameshiriki na mamia ya wananchi wa Mtaa wa Maseya-Kata ya Hombolo Makulu ujenzi wa Zahanati katika mtaa huo ikiwa ni utekelezaji wa ahadi aliyoitoa wakati wa Uchaguzi Mkuu 2025.

“Nawashukuru wananchi wa Maseya kwa kumchagua Rais Samia,mimi na Diwani wa kata yetu kwa kura nyingi sana kwenye uchaguzi mkuu uliomalizika.

Kazi yetu sasa ni kufanya kazi na kutatua changamoto za wananchi, tunawapongeza kwa kuitikia wito wa ujenzi wa zahanati yetu ambayo ofisi yetu iko kusogeza karibu huduma ya Afya kwa wananchi wetu.

Nitakabidhi kutuma 2000 na saruji mifuko 100 ili kulifikisha jengo letu mpaka hatua ya upauaji,ni imani yangu serikali yetu sikivu itatuunga mkono ukamilishaji wa zahanati hii”Alisema Mavunde.



Akitoa salamu za wananchi,Mwenyekiti wa Mtaa wa Maseya Alexander Fwalu amemshukuru Rais Samia S. Hassan kwa utekelezaji wa haraka wa ahadi ya umeme pamoja na uimbaji wa visima vya umwagiliaji kupitia Tume ya Taifa ya Umwagiliaji ambapo wananchi wengi wakulima watanufaika na kupata maji ya uhakika kwa ajili ya kilimo cha umwagiliaji.

Aidha pia Mwenyekiti Fwalu amemshukuru Mbunge Mavunde kwa kutimiza ahadi yake ya ujenzi wa ujenzi wa zahanati ya Maseya kwa uharaka na kuahidi wananchi wa Maseya wa kwamba watalazimika kuweka ujenzi wa ujenzi wa zahanati hiyo inakamilika kwa ajili ya hivyo kusogeza huduma ya Afya kwa wananchi.





Comments

Popular posts from this blog

WANAFUNZI WALIOMALIZA KIDIA SEKONDARI WACHANGIA UJENZI WA KANISA SH MILLION 20

VETA YAJIPANGA KUSHIRIKINA NA TOYOTA TANZANIA KUIMARISHA MAFUNZO YA UFUNDI MAGARI

UJENZI WA BWAWA LA KUFUA UMEME LA MTO MALAGARASI , WAPIGA HATUA MPYA