NDEJEMBI ASISITIZA UTEKELEZAJI WA VIPAUMBELE VYA SERIKALI KUFIKIA 2030



Asema  siku mia moja za Rais ni dira ya kufikia malengo

Asisitiza ushirikiano baina ya watumishi na viongozi ndani ya Wizara ya Nishati


Na Mwandishi wetu

WAZIRI wa  Nishati  Deogratius Ndejembi  amewaagiza Watumishi wa Wizara hiyo kufanya kazi kwa bidii ili kutimiza Vipaumbele vya Serikali katika Sekta ya Nishati ikiwemo kufikia Megawati 8000 ifikapo 2030.

Ndejembi ameyasema hayo tarehe 18 Novemba 2025 wakati akizungumza na watumishi wa Wizara mara baada ya kuwasili Katika Wizara  Mji  wa Serikali Mtumba Jijini Dodoma. 

Amesema watumishi wa Wizara ya Nishati ndio watendaji wakuu na wenye dhamana ya kuhakikisha kwamba malengo ya Serikali yaliyowekwa yanatimia kwa kufanya kazi kwa bidii , kuwataka watumishi kuchambua kwa kina  hotuba ya Mhe   Rais ili kuweza kufikia vipaumbele kwa wakati  na kuyoa huduma bora kwa wananchi wa Tanzania.




Pia amesisitiza watumishi kutumia siku mia moja za  Rais kama kipimo na  kielelezo cha kutathmini uelekeo wa malengo ya Serikali.

“Sisi kama viongozi wenu tunategemea zaidi ushirikano kutoka kwenu ninyi wataalamu wa hapa Wizara ya Nishati  ili tuweze kukamilisha Vipaumbele vya Rais alivyoviweka katika sekta yetu  kwasababu tunatakiwa tuanze kwa kukimbia na sio kutembea“ amesema Ndejembi.




Naye Naibu Waziri wa  Nishati Salome Makamba amewataka watumishi kushirikiana kwa pamoja na viongozi wa Wizara hiyo ili kuendesha Sekta ya Nishati kwa pamoja, na kuongeza kuwa anatambua kwamba maswala mengi ya sekta ya Nishati yameshafanyika tayari mpaka sasa.

Amesema  Serikali imeshafikisha Megawat 4000 za kiwango cha kuzalisha Umeme, hivyo ni jukumu letu kukamilisha miradi iliyokuwa inaendelea na kuongeza vyanzo vingine vya uzalishaji umeme ili kufikia megawati 8,000 ifikapo 2030.




Kwa upande wake Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati  Felchesmi Mramba amewashukuru viongozi hao na amewataka watumishi wa Wizara ya Nishati kutoa ushirikiano kwa viongozi hao sambamba na kutekeleza majukumu yao kwa wakati ili kuweza kutekeleza Vipaumbele vya Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan ifikapo mwaka 2030.







Comments

Popular posts from this blog

WANAFUNZI WALIOMALIZA KIDIA SEKONDARI WACHANGIA UJENZI WA KANISA SH MILLION 20

VETA YAJIPANGA KUSHIRIKINA NA TOYOTA TANZANIA KUIMARISHA MAFUNZO YA UFUNDI MAGARI

UJENZI WA BWAWA LA KUFUA UMEME LA MTO MALAGARASI , WAPIGA HATUA MPYA