PROF KABUDI: WIZARA YA HABARI NI MSINGI WA UMOJA NCHINI
Na Mwandishi wetu
WAZIRI wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Prof. Palamagamba Kabudi amesema wizara hiyo ina mchango katika msingi wa umoja na mshikamano wa Taifa unaosaidia kuleta maendeleo ya kijamii na Taifa kwa ujumla.
Kabudi amesema hayo Novemba 18, 2025 jijini Dodoma alipowasili katika Ofisi za wizara hiyo mara baada ya kuapishwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, Ikulu Chamwino, jijini Dodoma.
"Rais imempendeza kuturudisha kumsaidia katika wizara hii ambayo kwa ukubwa wake, ameteua Naibu Mawaziri wawili. Ni lazima tufanye kazi kwa ushirikiano na umoja ili tutimize azma ya kuwepo kwa wizara hii.
Ameongeza kuwa, wizara hiyo ndiyo wadau wakubwa wa Ofisi ya Rais, Maendeleo ya Vijana kwa sababu yanayotekelezwa hapo yanagusa vijana. Amewataka watendaji kusogea karibu zaidi na wananchi ili kuwasaidia katika kukua kwenye sekta hizo.
Kwa upande wake Naibu Waziri, Hamis Mwinjuma amesema kuwa, wakati huu ndio wa kufanya kazi zaidi ya kuwatumikia Watanzania na kuhakikisha wana furaha wakati wote na wanasaidiwa kukua na kunufaika na sekta hizo.
Naye Naibu Waziri, Paul Makonda ameshukuru kuwa sehemu ya kuongoza wizara hiyo muhimu kwa taifa.


Comments
Post a Comment