TANESCO MMEFANYA MAGEUZI MAKUBWA KATIKA HUDUMA YA UMEME KWA WANANCHI – NDEJEMBI
Aelekeza kuongeza kasi na ubunifu katika kuunganishia wananchi umeme
Asisitiza hatua kali za kisheria kwa wakandarasi wazembe
Na Mwandishi wetu,DODOMA
WAZIRI wa Nishati, Mhe. Deogratius Ndejembi, amesema kuwa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) limeendelea kufanya kazi kubwa katika kuboresha huduma ya umeme nchini hatua ambayo imeongeza imani na fursa za fursa kwa wananchi.
Ndejembi ameyasema hayo Novemba 22, 2025, mkoani Dodoma katika kikao chake na viongozi wa TANESCO chenye lengo la kupima na kukumbushana majukumu muhimu kuwahudumia wananchi. Ameutumia mkutano huo kuwataka watendaji wa TANESCO kuongeza kasi na ubunifu katika kuwaunganishia wananchi umeme kama sehemu ya utekelezaji wa Mpango Mkakati wa Misheni 300.
Amesema kuwa ili mpango huo utekelezeke ipasavyo, ni lazima kuwachukulia hatua wakandarasi wote watakaobainika kuwa wazembe au kushindwa kuendana na kasi ya serikali ya kuhakikisha kila Mtanzania ananufaika na huduma ya umeme.
“Nawapongeza TANESCO kwa kazi kubwa na nzuri ya kuwafikishia wananchi huduma ya umeme, lakini bado tuna kubwa mbele yetu. Ongezeni ubunifu na mbinu bora za kuwaunganishia wananchi umeme kwa haraka. Ninaamini tukishirikiana na wadau wetu, tutafikia lengo la kuwaunganishia wateja milioni 1.7 kwa mwaka,” Mhe. Ndejembi.
Naye Naibu Waziri wa Nishati Salome Makamba amemshukuru Rais. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuwekeza katika miradi ya umeme ambayo imekuwa na dhamira ya dhati ya kusaidia wananchi wote mijini na vijijini wanafikiwa na huduma ya umeme.
Kwa upande wake, Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati, Felchesmi Mramba, amesema TANESCO imekuwa ikitekeleza miradi yake kwa vya kimataifa, hatua fanya Tanzania kuwaletea mataifa mengine katika ujenzi na miradi inayoendelea ya miradi ya umeme.
Naye Makamu Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa TANESCO, Zuhura Bundala, Balozi Zuhura Bundala amesema Shirika hilo lina watendaji wazalendo na wenye kujituma, ambao wanaendelea kufanya kazi kwa bidii ambapo amesisitiza kwamba itaendelea na shirika ili kufikiria malengo yaliyowekwa.
Kwa upande wake, Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO, Lazaro Twange, amesema katika kipindi cha siku 100 za utendaji wa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, Shirika litakamilisha miradi ya umeme kwa kasi zaidi, ukiwemo mradi wa umeme wa jua wa Kishapu ambao kwa sasa umefikia asilimia 83 ya utekelezaji.
“Katika kipindi cha siku 100 za Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, tumejipanga baadhi ya miradi ya umeme inakamilika, ukiwemo mradi wa umeme wa Kishapu. Pia tunaendelea na mkakati wa kuwaunganishia wananchi lengo ni kuwafikia wateja milioni 1.7 kwa mwaka,” alieleza Bw. Twange.
Kikao kazi hicho kimehusisha viongozi wa ngazi ya juu ya TANESCO, wakurugenzi wa kanda, mameneja wa mikoa na wilaya, na kufunguliwa rasmi na Waziri wa Nishati, Mhe. Deogratius Ndejembi ambaye aliambatana na Naibu waziri wa nishati Mhe. Salome Makamba





Comments
Post a Comment