TANZANIA YAIHAKIKISHIA DUNIA HALI YA UTALII IKO SALAMA



Na Mwandishi Wetu, Riyadh

Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii, Dkt. Hassan Abbasi, akiongoza ujumbe wa Tanzania katika Mkutano wa 26 wa Baraza Kuu la Shirika la Utalii Duniani (UN Tourism) kilichoanza leo Novemba 9, 2025, jijini Riyadh, Saudi Arabia, nimeihakikishia dunia kuwa hali ya utalii na amani imara nchini Tanzania kufuatia machafuko yaliyotokea wakati baada ya uchaguzi katika baadhi ya maeneo.

Dkt. Abbasi ameyasema hayo leo wakati akichangia Taarifa ya Utekelezaji wa Mwaka wa Taasisi hiyo ambapo pia Tanzania ilinufaika na programu mbalimbali ikiwemo kuandaa Mkutano wa Dunia Kanda ya Afrika wa Utalii wa Vyakula vya Arusha April mwaka huu na kufadhiliwa baadhi ya programu za utunzaji wa mazingira katika maeneo ya Safu za Milima ya Usambara.

“Mheshimiwa Mwenyekiti wa Baraza hili baada ya kumpongeza Katibu Mkuu na Sekretarieti ya UN Tourism kwa utekelezaji ambao Tanzania pia imenufaika, naomba kutumia fursa hii kutoa taarifa kuwa Tanzania ni salama ya kadhia iliyojitokeza wakati wa uchaguzi.





Nawakaribisha wajumbe wa Mkutano na wadau wengine wa utalii kuja kutembelea kutembelea nchi hii ambayo ni kivutio bora Afrika kwa utalii wa safari,” alisema Dkt. Abbasi.

Aidha, mbali ya Tanzania kuwa miongoni mwa nchi 32 pekee kati ya wanachama wa Umoja huo wanaofikia 160 kuwa Mjumbe wa Kamati ya Utendaji (Executive Committe), leo pia Baraza Kuu hilo limeipitisha Tanzania kuwa Mjumbe wa Kamati ya Kuhakiki wanachama (UN Tourism Credentials Committe).

Mkutano huo unaendelea jijini hapa na pamoja na mambo mengine utajadili kuhusu matumizi ya akili unde katika kutangaza utalii na pia utachagua Katibu Mtendaji mpya.

Comments

Popular posts from this blog

WANAFUNZI WALIOMALIZA KIDIA SEKONDARI WACHANGIA UJENZI WA KANISA SH MILLION 20

VETA YAJIPANGA KUSHIRIKINA NA TOYOTA TANZANIA KUIMARISHA MAFUNZO YA UFUNDI MAGARI

UJENZI WA BWAWA LA KUFUA UMEME LA MTO MALAGARASI , WAPIGA HATUA MPYA