WASIMAMIZI WA ELIMU TAMISEMI KUWAJIBIKA KIKAMILIFU - KWAGILWA



Na Mwandishi wetu 

NAIBU Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (TAMISEMI),  Reuben Kwagilwa, amewataka watumishi wa Idara ya Elimu katika Ofisi hiyo kuhakikisha wanasimamia kikamilifu watendaji walio chini yao ili kuongeza ufanisi katika utoaji wa huduma.

Akizungumza na wasimamizi wa Idara ya Elimu katika Ofisi ya Waziri Mkuu – TAMISEMI Jjijini Dodoma Novemba 21, 2025 Kwagilwa amesema utekelezaji wa majukumu kwa weledi utasaidia kufikia malengo ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,  Dkt. Samia Suluhu Hassan ya kuendelea kuleta tabasamu kwa Watanzania kupitia maboresho ya sekta mbalimbali ikiwemo elimu. 

“Mheshimiwa Rais anatamani wizara hii ambayo inagusa wananchi moja kwa moja inapeleka tabasamu kwa watanzania hao lakini twendeni tukafanye udhibiti na tukatimize majukumu yetu kwa weledi kama ambavyo mmekuwa mkifanya siku zote.” 

Comments

Popular posts from this blog

WANAFUNZI WALIOMALIZA KIDIA SEKONDARI WACHANGIA UJENZI WA KANISA SH MILLION 20

VETA YAJIPANGA KUSHIRIKINA NA TOYOTA TANZANIA KUIMARISHA MAFUNZO YA UFUNDI MAGARI

UJENZI WA BWAWA LA KUFUA UMEME LA MTO MALAGARASI , WAPIGA HATUA MPYA