WASIRA AKIPONGEZA CHUO CHA MWALIMU NYERERE,AWATAKA VIJANA KUIBUA SULUHU ZA KITAIFA
Na Mwandishi wetu
MAKAMU Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Bara, Stephen Wasira, amewataka vijana wa kizazi kipya kutambua wajibu wao katika kulitumikia na kulijenga Taifa, akisisitiza kuwa Tanzania ndiyo nchi pekee wanayopaswa kuijivunia na kuithamini.
Wasira alisema hayo jijini Dar es Salaam wakati wa mahafali ya miaka 20 ya Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Julius Nyerere, ambako aliwasihi vijana kuachana na malalamiko yasiyo na tija na badala yake kutumia fursa zilizopo, hasa kutokana na kuanzishwa kwa Wizara ya Vijana.
"Malalamiko yasiyofuatwa na majibu hujenga hasira na jembe la watu kusema yao wenyewe. Haki kudaiwa kwa njia ya amani bila ghasia. Busara kutafuta chanya ili kupata suluhu za kitaifa," alisema.
Wasira alisema hakuna taifa lisilo na changamoto, akibainisha kuwa maendeleo hutatua matatizo ya zamani lakini pia huzalisha mapya, hivyo vijana kupokea mawazo ya matokeo nayo.
Aidha, aliipongeza menejimenti ya chuo kwa hamafali hayo muhimu, kusema taasisi hiyo imeendelea kuwa chachu ya kuwasilisha ujumbe na viongozi watarajiwa wa Taifa. Pia aliuomba uongozi wa chuo kuendelea programu za umahiri na uzamili kwa mustakabali mzuri wa taasisi hiyo.
Katika hatua nyingine Wasira aliwatia moyo kwa hatua waliyofikia, akiwapongeza kwa nidhamu, uzalendo na umahiri waliouonesha katika kipindi chote cha masomo.
"Taarifa ya chuo inaonesha kuwa, pamoja na taaluma mliyopata, mmefundishwa uongozi na uzalendo. Huwezi kuipenda nchi bila kuijua, kuithamini na kuithamini kwa kutoa mawazo ya kuijenga," alisema.
Kwa upande wake, Mkuu wa hicho, Profesa Haruni Mapesa, kimeendelea kupata heshima kitaifa na kimataifa, chuo kama kituo cha mitihani ya Kiingereza.
Alibainisha kuwa idadi ya wanafunzi imeendelea kukua hadi mwaka katika kampasi ya Kivukoni, kutoka 11,576 2023/2024 hadi 12,197 mwaka 2024/2025, na gazeti linatarajiwa kwa mwaka zaidi wa masomo 2025/2026.
Mapesa alisema jumla ya wahitimu 5,255 wametunukiwa vyeti mbalimbali, ambapo wanawake ni 2,410 sawa na asilimia 46, huku wanaume wakiwa 2,845 sawa na asilimia 54.
Aliongeza kuwa miongoni mwa wahitimu, wapo wahitimu wa shahada za umahiri, akiwemo tisa wa Shahada ya Urasilimiali Watu na 11 wa Shahada ya Umahiri katika Uongozi, Maadili na Utawala.






Comments
Post a Comment