WAZIRI NDEJEMBI AKABIDHIWA OFISI NA ALIYEKUWA NAIBU WAZIRI MKUU NA WAZIRI WA NISHATI DKT. BITEKO

 


Na Mwandishi wetu

WAZIRI wa Nishati, Deogratius Ndejembi leo tarehe 20 Novemba, 2025, amekabidhiwa rasmi ofisi na aliyekuwa Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mheshimiwa Dkt. Doto Mashaka Biteko kwenye ofisi za Wizara zilizoko mtumba mkoani Dodoma, na kumshukuru Mhe. Biteko kwa utendaji wake wa kazi katika kipindi chote cha uongozi wake.

Waziri Ndejembi amesema katika kipindi cha uongozi wake, kwenye sekta ya nishati umekuwa kwa kiasi kikubwa na huduma za utendaji kazi zimeboreshwa na kuona harakati za sekta ya nishati.

Waziri Ndejembi ameahidi atayaendeleza pale alipoishia Mhe.Biteko, ili kusaidia azma ya serikali na maononayo malengo ya miradi ifikapo 2030 yanafikiwa.






Kwa upande wake, Dkt. Biteko amempongeza Mhe. Deogratius Ndejembi kwa kuteuliwa kuwa Waziri wa Nishati na kumhakikishia wakati wowote mazungumzo makubwa ya Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan katika Sekta ya Nishati

 “ Mengi niliyojifunza kipindi nikiwa Wizara ya Nishati lakini jambo kubwa zaidi ni sala zangu kwenu katika utekelezaji wa kazi zenu za kila siku “ amesema Biteko. 



Halfla ya Makabidhiano hayo imehudhuriwa na Naibu Waziri wa Nishati, Mhe. Salome Makamba, Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati, Mha. Felchesmi Mramba, pamoja na viongozi waandamizi kutoka Wizara ya Nishati.


Comments

Popular posts from this blog

WANAFUNZI WALIOMALIZA KIDIA SEKONDARI WACHANGIA UJENZI WA KANISA SH MILLION 20

VETA YAJIPANGA KUSHIRIKINA NA TOYOTA TANZANIA KUIMARISHA MAFUNZO YA UFUNDI MAGARI

UJENZI WA BWAWA LA KUFUA UMEME LA MTO MALAGARASI , WAPIGA HATUA MPYA