KAULI YA ASKOFU RUWA'ICHI ZAWAIBUA WAUIMINI

 



Na Mwandishi Wetu

BAADHI ya waumini wa Kanisa wamejitokeza hadharani kupinga vikali kauli walizodai kuwa ni za matusi, vitisho na hukumu zilizotolewa na Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu la Dar es Salaam, Jude Thaddaeus Ruwa'ichi, wakisema zimetumika vibaya madhabahuni na kujeruhi imani ya waumini.

Wakizungumza na waandishi wa habari Jijini Dar es salaam mapema leo Desemba 27, 2025, waumini hao Mackdeo Shilinde na Gerald Abel wamesema kauli zilizotolewa na Askofu Ruwa'ichi wakati wa homilia ya Misa Takatifu ya Krismasi tarehe 25 Desemba 2025 zimekiuka misingi ya mafundisho ya Kikristo na maadili ya uongozi wa kiroho. 

Wabadala ya kujibu hoja halali zilizowasilishwa kwa Balozi wa Vatican, Askofu alitumia mimbari kueneza lugha waliyoitaja kuwa ya chuki, hofu na udhalilishaji wa waumini.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo, mimbari ya Kanisa Katoliki ni mahali patakatifu palipokusudiwa kuhubiri Neno la Mungu, imani, kuwafariji waumini na kuwa katika njia ya mapendo, uvumilivu na mshikamano, na si jukwaa la kushambulia dhamira za waumini au kuwavua hadhi yao ya Ukristo hadharani.

hiyo imeeleza kuwa Askofu Ruwa'ichi alitumia maneno mazito- maneno ambayo waumini hao wamesema hayana nafasi katika mahubiri ya Kikristo yanayopaswa kuongozwa na upendo na haki. Wamesema matumizi ya lugha hiyo yanakwenda kinyume na mafundisho ya Yesu Kristo yanayokataza kuhukumu watu hadharani. 


Comments

Popular posts from this blog

WANAFUNZI WALIOMALIZA KIDIA SEKONDARI WACHANGIA UJENZI WA KANISA SH MILLION 20

VETA YAJIPANGA KUSHIRIKINA NA TOYOTA TANZANIA KUIMARISHA MAFUNZO YA UFUNDI MAGARI

UJENZI WA BWAWA LA KUFUA UMEME LA MTO MALAGARASI , WAPIGA HATUA MPYA