MRADI WA USAMBAZAJI UMEME VITONGOJINI SIHA-KILIMANJARO WAZINDULIWA



Lengo la mradi ni kuunganishia umeme kaya 5,000 ifikapo 2030

Kaya 3000 tayari zimefaidika na mradi

Salome asema dhamira ya Rais Samia ni kuiangaza Tanzania nzima kwa nishati ya umeme

Asema mpango wa Misheni 300 unatekelezwa kwa kasi Tanzania

Na Mwandishi Wetu

NAIBU Waziri wa Nishati, Salome Makamba amezindua mradi wa umeme katika vitongoji vya Wilaya ya Siha mkoani Kilimanjaro, akisisitiza kuwa Serikali itaendelea kutekeleza dhamira ya Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan ya kuhakikisha wananchi wote wanafikiwa na huduma ya umeme.

Mawasiliano wilayani Siha, wakati wa hafla ya mawasiliano, Makamba amesema kuwa pamoja na umeme kuunganishwa kwenye kaya, Wizara ya Nishati inaendelea kuhifadhi taasisi za umma, hususan shule, zinaunganishwa pia na umeme ili kuboresha mazingira ya kujifunzia na kufundishia.

Katika hafla hiyo, Naibu Waziri aliwasha rasmi umeme katika Kitongoji cha Ngare-Nairobi na kueleza kuwa, "tumeanza na kitongoji hiki lakini katika Wilaya ya Siha pekee Serikali inatekeleza mpango wa kuwasha umeme kwa kaya 5,000 ifikapo mwaka 2030. Hadi sasa kaya 3,000 tayari zimeunganishwa na umeme."



Katika hatua nyingine, Salome amesema Tanzania inaendelea kutekeleza kwa kasi Mpango Mahsusi wa kuwafikishia umeme Waafrika Milioni 300 ifikapo mwaka 2030 (Mission 300) ukiwa na lengo la kulinda wananchi wote nchini wanafikishwa na huduma ya umeme ifikapo mwaka wa 2030.

"Kupitia Mpango wa Misheni 300, TANESCO inalenga kuunganishia umeme wananchi 1,700,000 kwa mwaka ambapo Mkoa wa Kilimanjaro pekee unalenga kuunganisha wananchi 12,000 kwa mwaka na hadi sasa zaidi ya wananchi 9,000 tayari wamepata huduma ya umeme mkoani humu." Amesema





Kwa upande wake, Meneja wa TANESCO Mkoa wa Kilimanjaro,  Merry Kabakuzi amesema Wilaya ya Siha ina jumla ya vitongoji 169 ambapo vitongoji 155 tayari vina umeme huku vitongoji 14 vilivyosalia vikiwa katika Mpango wa Wakala wa Nishati Vijijini (REA) awamu ya pili ya ujazilizi wa vitongoji.

Ameeleza kuwa maeneo ambayo umefika kwa kiwango kidogo yataendelea kuongezwa mtandao kupitia Mpango Mahsusi wa misheni 300.





Comments

Popular posts from this blog

WANAFUNZI WALIOMALIZA KIDIA SEKONDARI WACHANGIA UJENZI WA KANISA SH MILLION 20

VETA YAJIPANGA KUSHIRIKINA NA TOYOTA TANZANIA KUIMARISHA MAFUNZO YA UFUNDI MAGARI

UJENZI WA BWAWA LA KUFUA UMEME LA MTO MALAGARASI , WAPIGA HATUA MPYA