NAIBU WAZIRI MAKAMBA AIPONGEZA PBPA KWA UTENDAJI KAZI MZURI






Na Mwandishi Wetu - Dar es Salaam 

NAIBU Waziri wa Nishati, Salome Makamba (Mb) ameipongeza Wakala wa Uagizaji Mafuta kwa Pamoja (PBPA) kwa utendaji mzuri katika suala hili inakuwa mafuta ya kutosha.

Ameyasema hayo wakati. na Menejimenti ya PBPA leo Desemba 6,2025 jijini Dar es Salaam.

"Nawapongeza kwa kazi nzuri mnayoifanya lakini hakikisheni mnatoa elimu kwa Watanzania kuhusu majukumu yenu na kazi zenu" amesema Salome.



Ametumia kuitaka PBPA kuwawezesha Watanzania wazawa kuingia kwenye biashara ya mafuta na kufanya kazi kwa nafasi hiyo.

"Lazima tupate wa Tanzania, tuwawezeshe waingie kwenye biashara hii" amesisitiza Mhe. Salome.

Naye, Mkurugenzi Mkuu wa Wakala wa Uagizaji Mafuta kwa Pamoja (PBPA), Bw. Erasto Simon amesema wakala hiyo imefanikiwa kufanikiwa kunakuwa na akiba ya mafuta ya kutosha, uwepo wa data sahihi za kiasi cha mafuta pamoja na kuiwezesha Serikali kuandaa kuandaa.

"Mfumo wa Bulk Procurement System (BPS) umesaidia hata nchi za jirani kuagiza mafuta kwa karibia asilimia 95 sambamba na kudhibiti ubora wa bidhaa za mafuta yanayoingia nchini.


Amefafanua kuwa nchi za jirani kama Malawi, Zambia, Uganda, Rwanda, Zimbabwe na Namibia wanaendelea kutembelea Tanzania na kujifunza kuhusu namna bora ya uagizaji mafuta katika nchi zao.

Amesema PBPA imefanikiwa kuratibu uagizaji mafuta kwa ufanisi mkubwa kutokana na uwazi uliopo katika mchakato mzima wa uagizaji mafuta.

Lengo la ziara ya  Makamba katika ofisi za PBPA ni kujifunza kuhusu majukumu ya PBPA pamoja na kutambulisha mara baada ya kuteuliwa na Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuwa Naibu Waziri katika Wizara ya Nishati.

Comments

Popular posts from this blog

WANAFUNZI WALIOMALIZA KIDIA SEKONDARI WACHANGIA UJENZI WA KANISA SH MILLION 20

VETA YAJIPANGA KUSHIRIKINA NA TOYOTA TANZANIA KUIMARISHA MAFUNZO YA UFUNDI MAGARI

UJENZI WA BWAWA LA KUFUA UMEME LA MTO MALAGARASI , WAPIGA HATUA MPYA