NGORONGORO YAENDELEA KUJENGA UWEZO WA UTENDAJI KAZI KWA WATUMISHI WAKE.





Na Mwandishi wetu.

MAMLAKA ya Hifadhi ya Ngorongoro imeendelea kuwajengea watumishi wake kwa kuwapa mafunzo ya namna bora zaidi masuala ya Itifaki na kuhudumia wageni mbalimbali wanaotembelea hifadhi hiyo.

Akifungua mafunzo kwa Maafisa Uhusiano kwa Umma wa Mamlaka hiyo jijini Mwanza Mshauri wa Jeshi la Uhifadhi Ngorongoro Kanali Fikiri Machibya ameeleza kuwa muhimu kwa viongozi kwa umma wa mamlaka hiyo kujiimarisha katika masuala ya mawasiliano na itifaki za kijeshi ili kuimarisha kazi yao na kufikiria mawazo yake juu ya mipango yake.

“Tunataka kuendelea kuwa Premium Safari Destination katika taasisi yetu, hivyo ni muhimu kubadilika na kupeana mafunzo ya mara kwa mara kwa ubunifu, maarifa na nidhamu maeneo ya kazi ili wageni tunaowahudumia wafurahie huduma zetu na kutangaza maeneo yote duniani”alisema Kanali Machibya.


Kaimu Meneja Uhusiano kwa Umma wa Mamlaka hiyo Hamis Dambaya amesema kuwa mafunzo hayo yeye na timu yake kujijengea uwezo watumishi wa kitengo hicho katika kipindi hiki ambacho mamlaka hiyo imedhamiria kufanya mabadiliko makubwa katika utendaji na kihuduma.

Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro imeendelea kuwa kivutio bora barani Afrika kutokana na umahiri wake katika shughuli zote za uhifadhi, utalii na maendeleo ya jamii jambo ambalo limekuwa likivutia wageni wengi kutoka kutembelea kutembelea vivutio vya utalii vilivyopo.




Comments

Popular posts from this blog

WANAFUNZI WALIOMALIZA KIDIA SEKONDARI WACHANGIA UJENZI WA KANISA SH MILLION 20

VETA YAJIPANGA KUSHIRIKINA NA TOYOTA TANZANIA KUIMARISHA MAFUNZO YA UFUNDI MAGARI

UJENZI WA BWAWA LA KUFUA UMEME LA MTO MALAGARASI , WAPIGA HATUA MPYA