RIADHA ILIVYOING'ARISHA NGORONGORO KAMA PREMIUM SAFARI DESTINATION KWENYE MASHINDANO YA SHIMMUTA
Na Mwandishi wetu
MCHEZO wa riadha umeonyesha kuwa ni muhimu zao la michezo Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro kutokana na kupata mchezo huo kutoka Ngorongoro kuzoa jumla ya medali saba (07) pamoja na ushindi wa mbio za kupokezana vijiti.
Timu ya Ngorongoro ya riadha ilinogesha mashindano hayo kwa wakimbiaji wake kuonesha vipaji vya hali ya juu zaidi kudhirisha kuwa Ngorongoro ni Premium Safari Destination.
Katika salamu zake kwa wanamichezo wote wa Ngorongoro Kamishna wa Mamlaka hiyo Bwana Abdul-Razaq Badru amewapongeza kutokana na kushiriki kwenye michezo na kutangaza vivutio vya utalii vilivyopo Ngorongoro pamoja na nidhamu na uwajibikaji wakati wote wa mashindano.



Comments
Post a Comment