URITHI NGORONGORO: FAHAMU UTARATIBU WA MSIBA NA MAZIKO KWA KABILA LA WAHADZABE



Na Mwandishi wetu 


JAMII ya kabila la Wahadzabe ina historia ya kuvutia katika kila nyanja ya maisha yao, watalii mbalimbali wanaotaka kujua hadithi nzuri za kuvutia,kusisimua na kuelimisha kuhusu mila, desturi, utamaduni na historia ya wahadzabe huwatembelea katika makazi yao yaliyopo pembezoni mwa Ziwa Eyasi. 

Vilevile kwa mgeni au mtalii yoyote akitembelea Makumbusho ya kisasa ya Ngorongoro Lengai UNESCO Jiopaki (Urithi Geopark Museum) inayosimamiwa na Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro Wilayani Karatu basi atapata hadithi nzuri na maelezo ya kutosha kuhusu masuala yote ya kabila hili. 



Baada ya wiki mbili zilizopita kuchapisha makala zenye hadithi kuhusu kichwa cha nyani na thamani yake katika ushenga na harusi kwa kabila la wahadzabe pamoja na makala iliyohusu adhabu ya kuchepuka katika kabila hilo, wiki hii tutaangazia utaratibu wa mazishi unavyofanyika katika kabila hilo lililotunza historia ya utamaduni na maisha yake. 

Wapo baadhi ya watu wanaamini kuwa Wahadzabe huwa hawafi na badala yake hupotea tu hasa kutokana na maisha yao ya kuishi msituni kwa kula Nyama, mizizi na matunda na kwamba jamii hiyo haina mila ya mazishi kama jamii zingine, laaah hasha!!.



Ukweli ni kwamba Wahadzabe hufa kama walivyo binadamu wengine na pia katika maisha yao huamini kuwa mtu akifa huwa ameitwa na Mungu wao (HEPEME) wanayeamini kuwa Mungu huyo anaishi kati jua na mwezi na ndiye huwa anawapa baraka katika maisha yao ya kila siku.

Kwa mujibu wa mzee Shagembe Gambai ambae ni Kiongozi wa kabila la Wahadzabe kutoka katika kijiji cha Eyasi Ngorongoro anaeleza kuwa Mungu wao ni mwenye huruma na baraka na ndio maana mtu akifa katika kabila lao huamini kuwa ameenda kwa Mungu wao anayejulikana kama Ishoko au Hepeme.

Mzee Shagembe anafafanua kuwa Wahadzabe huamini kuwa jua na mwezi ni vitu vyenye nguvu sana na huonesha uwezo wa muumba katika kuwapa chakula chao cha kila siku, ambapo maombi yao makuu kwa Mungu (Hepeme) ni kuomba awajalie mawindo na kuwaepusha na majanga yote, mwisho kifo ambacho ni lazima wakipitie. 

Comments

Popular posts from this blog

WANAFUNZI WALIOMALIZA KIDIA SEKONDARI WACHANGIA UJENZI WA KANISA SH MILLION 20

VETA YAJIPANGA KUSHIRIKINA NA TOYOTA TANZANIA KUIMARISHA MAFUNZO YA UFUNDI MAGARI

UJENZI WA BWAWA LA KUFUA UMEME LA MTO MALAGARASI , WAPIGA HATUA MPYA