UWEKEZAJI MKUBWA ULIOFANYWA NA SERIKALI KITUO CHA GESI ASILIA MLIMANI WALETA NAFUU KWA WANANCHI



Kituo kina uwezo wa kujaza gesi asilia kwenye magari na bajaji 800 kwa siku

Salome Makamba ahamasisha Sekta binafsi kuwekeza katika eneo la gesi asilia

Mikoa ya Morogoro, Dodoma, Arusha, Kilimanjaro na Tanga kufikiwa na vituo vya gesi asilia

Na Mwandishi wetu

NAIBU waziri wa Nishati Mhe.Salome Makamba ameeleza kuwa, Serikali imefanya uwekezaji mkubwa katika kujenga kituo cha kujaza gesi asilia kwenye vyombo vya usafiri katika eneo la Mlimani jijini Dar es Salaam ambapo zaidi ya sh.Bilioni 12 zimetumika kukamilisha kituo hicho chenye uwezo wa kuhudumia magari madogo na bajaji 800 kwa siku.

Salome amebainisha hayo Novemba 12, 2025 Jijini Dar es Salaam wakati wa ziara yake ya kukagua kituo hicho kinachosimamiwa na Kampuni Tanzu ya Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania(TPDC) ya GASCO.

Salome ameeleza kuwa Serikali ya Tanzania inayoongozwa na Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan inahakikisha rasilimali zilizopo zinawanufaisha wananchi kwa namna mbalimbali.



“Matumizi ya gesi asilia iliyoshindiliwa (CNG) yamerahisisha gharama za maisha kwa watu wa vyombo vya usafiri kwani gharama ya gesi kilo moja ni shilingi 1500 ambapo ukiwa na mtungi wa Kilo 17 unaweza kusafiri umbali wa KM 50 hii inaonesha dhahiri kuwa gesi inagharama nafuu zaidi kuliko mafuta lakini pia kutokana na wingi wa magari ya biashara na bajaji katika mkoa wa Dar es Salaam uwekezaji huu umekuwa ni fursa kwa wafanyabiashara hao katika kupunguza gharama za uendeshaji na kuongeza kipato.” Amesema Salome

Ameeleza kuwa, hadi kufikia Juni 2026 kutakuwa na vituo vingine vya kujaza gesi katika maeneo ya kila barabara kubwa ya Mkoa wa Dar es Salaam huku akisiaitiza kuwa Serikali pia imeanza mpango wa kujenga vituo vikubwa katika Mikoa ya Morogoro, Dodoma, Arusha, Kilimanjaro na Tanga ambavyo vitasaidia wananchi wa mikoa hiyo kupata huduma lakini pia wananchi wa Mikoa ya karibu kunufaika na huduma husika.


Salome ametoa wito kwa sekta binafsi kuongeza kasi ya uwekezaji katika miundombinu ya gesi asilia, akibainisha kuwa mahitaji ya nishati nafuu yanaongezeka kwa haraka nchini hivyo n

Comments

Popular posts from this blog

WANAFUNZI WALIOMALIZA KIDIA SEKONDARI WACHANGIA UJENZI WA KANISA SH MILLION 20

VETA YAJIPANGA KUSHIRIKINA NA TOYOTA TANZANIA KUIMARISHA MAFUNZO YA UFUNDI MAGARI

UJENZI WA BWAWA LA KUFUA UMEME LA MTO MALAGARASI , WAPIGA HATUA MPYA