WANAHARAKATI WAOMBA MSAADA KUENEZA ELIMU YA UZALENDO
Na Mwandishi Wetu
WANAHARAKATI Ahmed Kombo na Joseph Yona wameomba, kutuma pamoja na Serikali kwa ujumla kuwaunga mkono ili waweze kutekeleza ziara za kitaifa za kueneza elimu ya uzalendo, umuhimu wa amani kwa Taifa pamoja na uhamasishaji wa vijana kuhusu fursa mbalimbali zinazopatikana nchini.
Wakizungumza na waziri wa habari jijini Dar es Salaam mapema leo Januari 7, 2026, Kombo amesema lengo la ziara hiyo ni kuweka na baadhi ya baadhi ya wasiolitakia taifa mema wanaodaiwa kuwapotosha vijana kwa nia ya kuchafua amani ya nchi.
Amesema ya Tanzania imejengwa kwa historia ndefu ya mshikamano na amani, hivyo ipo haja ya kuendelea kuwaelimisha vijana juu ya wajibu wao wa kulinda amani hiyo.
“Lengo kuu la ziara hiyo ni kutoa elimu kwa vijana kuhusu namna ya kutunza amani pamoja na kuwapa mbinu mbalimbali za kulinda nchi yao,” amesema Kombo.
Aidha, ameiomba Serikali pamoja na wananchi wenye mapenzi mema kuwawezesha ziara hiyo ili waweze kuwafikia vijana wengi zaidi nchini.
Kombo amesema wananchi wanaoguswa na mpango huo wanaweza kuchangia kupitia akaunti ya NMB iitwayo Josepha and Ahmed, namba 24510065664.
Kwa upande wake, Joseph Yona amesema vijana watachangamkia fursa mbalimbali zinazotolewa Serikali ili kujikwamua kiuchumi.
Amebainisha kuwa Serikali imeweka kipaumbele katika kutoa mikopo kwa vijana, hivyo ni wakati kwa vijana matumizi mikopo hiyo kuleta maendeleo binafsi na ya taifa kwa ujumla.



Comments
Post a Comment