WANANCHI KATA YA BUYUNI WAJITOKEZA KWA WINGI KUPATA VITAMBULISHO VYA NIDA
Na Mwandishi Wetu
WANANCHI wa Kata ya Buyuni, Jimbo la Ukonga, Jijini Dar es Salaam, wamejitokeza kwa wingi katika Ofisi ya Mtendaji wa Kata hiyo kushiriki zoezi la kupata Vitambulisho vya Taifa (NIDA), hatua inayolenga kuwawezesha kupata fursa mbalimbali kama mikopo kutoka taasisi za kifedha.
Akizugumza na waandishi wa habari Jijini Dar es salaam katika uzinduzi wa zoezi hilo,mapema leo Januari 19,2026 Diwani wa Kata ya Buyuni, Jesca Msolla, amesema utoaji wa vitambulisho hivyo umetokana na maombi kutoka kwa wananchi waliokuwa wakikosa fursa za mikopo kwa kukosa kitambulisho cha Taifa, hali iliyokuwa ikiwakwamisha.
"Uamuzi wa kuleta huduma hii na wananchi unalenga kumbukumbu na wananchi katika kata ya buyuni ambao walikuwa wakija Ofisi kwa ajili ya kuomba msaada wa kupata NIDA"amesema
Amesema katika zoezi hilo hadi sheya mchana mchana wananchi 200 taarifa zao zimefanyiwa kazi na mamlaka zote muhimu ambazo zimeshiriki pamoja NIDA, wanasheria pamoja na Idara ya Uhamiaji ili kusaidia wananchi wanahudumiwa ipasavyo.
Kwa upande wake, Balozi wa Uwamasishaji wa zoezi hilo, Heri Shaban, amesema zoezi la zoezi limezinduliwa Leo Januari 19,2026 katika kata ya buyuni na Chanika na kuona tamati Januari 30, 2026.
Aidha amewaomba wananchi wote wa Jimbo la Ukonga, hususani Kata za Buyuni, Chanika, Zingiziwa na maeneo ya jirani, kujitokeza kwa wingi kupata huduma hiyo ili kuhakikisha kila mwananchi anatambulika na anapata kitambulisho cha Taifa.







Comments
Post a Comment