BoT YAONYA MATUMIZI YA NOTI KUTENGENEZEA MAUA




Na Mwandishi wetu.

BENKI Kuu ya Tanzania (BoT) imetoa onyo kali kwa wananchi wanaotumia fedha kama mapambo au zawadi za Valentine, ikisema ni kinyume cha sheria na kunasababisha uharibifu wa noti.

Akizungumza Dodoma, Gavana wa BoT,  Emmanuel Tutuba, amesema matumizi hayo yamekuwa yakiongezeka katika kipindi cha sikukuu, hali inayosababisha hasara kubwa kwa Taifa.

Amesema noti zinazofungwa kwenye mashada ya maua hupoteza ubora wake kutokana na gundi na mikunjo, na hivyo kushindwa kutumika kwa muda mrefu.

“Fedha ni alama ya Taifa. Kila Mtanzania ana wajibu wa kuzilinda,” amesema.

BoT imewataka wananchi kutumia njia mbadala za kutoa zawadi, ikiwemo bidhaa au fedha zilizo katika hali yake halisi.

Comments

Popular posts from this blog

WANAFUNZI WALIOMALIZA KIDIA SEKONDARI WACHANGIA UJENZI WA KANISA SH MILLION 20

VETA YAJIPANGA KUSHIRIKINA NA TOYOTA TANZANIA KUIMARISHA MAFUNZO YA UFUNDI MAGARI

UJENZI WA BWAWA LA KUFUA UMEME LA MTO MALAGARASI , WAPIGA HATUA MPYA