KAMATI YA BUNGE YAITA WAWEKEZAJI UJENZI WA VITUO VYA GESI ASILIA ILIYOSHINDILIWA (CNG)

 





Yapongeza kasi ya Ujenzi wa vituo vya CNG*

Na Mwandishi wetu 

KAMATI ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini, kupitia Mwenyekiti wake Mhe. Subira Mitalu, imetoa wito kwa kuunga mkono Serikali katika ujenzi wa vituo vya gesi asilia iliyoshindiliwa (CNG) ili kurahisisha upatikanaji wa huduma hiyo kwa wananchi katika Jiji la Dar es Salaam na mikoa mingine inayojumuisha Morogoro na Dodoma.

Wito huo umetolewa tarehe 19 Februari 2026 wakati Kamati hiyo ilipotembelea Kituo Mama cha Gesi Asilia Iliyoshindiliwa (CNG) kilichopo eneo la Mlimani jijini Dar es Salaam.

“Tumeona tayari ina mpango wa kuongeza ujenzi wa Serikali hivi kutokana na uendelezaji wa wananchi kuendelea kukua pamoja na unafuu unaopatikana unaotumia CNG kwenye vyomvbo vya usafiri kama vile magari na bajaji, kwani gharama zinapungua kwa asilimia 40 ukilinganisha na mafuta. Mgalu




Aidha, kamati hiyo imetoa wito kwa Serikali kufunga mfumo wa CNG katika magari yake, jambo litakalosaidia gharama za vyombo vya habari na usafiri.

Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini pia imeipongeza Serikali kupitia Wizara ya Nishati na Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) kwa ujenzi inaoufanya katika ujenzi wa vituo vya CNG na kupelekea vyombo vya usafiri vipatavyo 15,000 kutumia CNG.

Vilevile, imepongeza shughuli za utafiti na uendelezaji wa gesi asilia zinazoendelea; ikisema kuwa upatikanaji wa gesi asilia ya kutosha itawezesha kuboresha huduma nyinginezo kama vile majumbani na viwanda.




Kwa upande wake, Naibu Waziri wa Nishati, Salome Makamba, amesema tangu kuanza kwa vituo vya CNG nchini, Serikali imekuwa ikiona kazi zake na ndiyo maana inaongeza kasi ya usogezaji huduma hiyo kwa wananchi kwa kuhusisha pia sekta binafsi mfano ukiwa ni kitengo cha hivi karibuni kituo cha CNG cha Puma kilichopo Salasala ambacho Afrika ndicho chanzo kikubwa.

Amesema Serikali pia katika mwaka huu wa fedha imeagiza magari makubwa matano yatakayobeba gesi asilia iliyoshindiliwa na kusambaza vituo vilivyopo katika maeneo ya mbali mbali Dodoma, Morogoro, Arusha na Tanga, lengo likiwa ni kuhakikisha huduma hiyo iko eneo moja kwenda nyingine.

Kuhusu kubadilisha mfumo wa magari ya Serikali kwenda kwenye CNG, ameeleza kuwa, tayari Serikali imeanza kufanyia kazi suala hilo na moja ya vielelezo ni mabasi mapya ya mwendo kasi ambayo yote yanatumia mfumo wa CNG, jambo ambalo limefanya utoaji wa huduma kwa abiria.

Kituo cha CNG Mlimani kina uwezo wa kubadilisha gesi asilia kwenye magari 1,200 kwa siku huku kikiwa na pampu maalum kwa ajili ya kununua magari maalum ya kusafirisha CNG kwenda vituo vidogo vya gesi kwenye magari (Offline CNG Filling Stations), viwandani, katika taasisi na majumbani.


Comments

Popular posts from this blog

WANAFUNZI WALIOMALIZA KIDIA SEKONDARI WACHANGIA UJENZI WA KANISA SH MILLION 20

VETA YAJIPANGA KUSHIRIKINA NA TOYOTA TANZANIA KUIMARISHA MAFUNZO YA UFUNDI MAGARI

UJENZI WA BWAWA LA KUFUA UMEME LA MTO MALAGARASI , WAPIGA HATUA MPYA