MAFUNDI NA WAUNDAJI VIPIMO NCHINI WAASWA KUENDANA NA TEKNOLOJIA

 



WMA - Dodoma

MAFUNDI wa vipimo, waundaji wa mizani pamoja na wapimaji wa matanki ya kuhifadhi mafuta ardhini wameshauriwa kuelekeza katika vipimo vya kidijitali kutokana na maendeleo ya teknolojia yanayoleta mabadiliko kila siku.

Wito huo umetolewa na Mkurugenzi wa Huduma za Ufundi, Wakala wa Vipimo (WMA), Francis Olwero, wakati wa kikao kazi na mafunzo kwa kundi hilo, yaliyoandaliwa na Ofisi ya WMA Mkoa wa Dodoma na kufanyika Februari 18, 2026.

Akifungua kikao kazi na mafunzo hayo, Mkurugenzi Olwero aliwaambia wanafunzi kuchukua katika teknolojia kunailazimu sekta ya vipimo na mabadiliko yanayotokea ili kazi ziendelee kufanyika.




Mkurugenzi wa Huduma za Ufundi kutoka Wakala wa Vipimo (WMA), Bw. Francis Olwero na mafundi na waundaji wa vipimo wakati kikao kazi kilichofanyika baina yao na WMA Mkoa wa Dodoma Februari 18, 2026 Dodoma kwa lengo la masuala muhimu kuhusu sekta hiyo.

“Mathalani, kanuni ya zamani ya kuomba leseni imebadilika, kwahiyo nanyi tayari kubadilika Sasa hivi mambo mengi ni ya ki-elektroniki, usikubali kubaki nyuma,” alisisitiza

Akichanganua zaidi, Mkurugenzi Olwero alitahadharisha kuwa kutokana na mabadiliko ya kiteknolojia, katika kipindi cha miaka michache ijayo, vipimo visivyo vya ki-elekroniki kama vile mizani vitakuwa havitumiki tena hivyo akawashauri mafundi na waundaji wa vipimo hivyo kufanya wanatumia muda wa kujifunza na kuwekeza kwenye vile vile vya ki-elekroniki ili kwenda sokoni.

"Jaribuni kujifunza kutengeneza mizani za kielektroniki. Muda sio mrefu mtaona hizi za kawaida hazitumiki tena. Kwahiyo, kama unataka kufanya kazi ya ufundi wa miaka ijayo, uwe umeshabobea kwenye elektroniki."

Katika hatua nyingine, aliwashauri mafundi na waundaji wa vipimo vya kufanya kazi kwa kuweka baina yao lakini pia kutoa msaada kwa Maafisa wa WMA walioko katika maeneo yao ili kuhakikisha kazi inafanyika kwa mujibu wa sheria na kila kundi linanufaika ipasavyo.

Akifafanua, aliwataka kujitambulisha kwa Meneja wa WMA wa eneo husika wakati wanapoenda kufanya kazi ili uwepo wao katika eneo hilo utambuliwe.

“Itamsaidia Meneja kuthibitisha kama leseni yako ni halali ili yeye pia aweze kupata changamoto za kazi. Hiyo itakusaidia pia kufanya kazi yako ujasiri na kujiamini,” alisisitiza Mkurugenzi.

Mafunzo kwa niaba ya viongozi, Mwenyekiti wa Umoja wa Mafundi Mizani Dodoma, Shaidu Rwemuka alipongeza jitihada ambazo zimekuwa zikifanywa na WMA Mkoa wa Dodoma kwa kupanga vikao vya mara kwa mara akisema vinasaidia kuwajengea uwezo wa kufanya kazi kwa ufanisi na nidhamu.

Aidha, kuhusu kuanzishwa kwa Mfumo huo mpya wa kielektroniki, Rwemuka alisema kuwa kumesaidia mambo mengi kuokoa muda.

“Awali, ilikua ukusanye taarifa, uende sehemu mbalimbali ikiwemo WMA na BRELA na baada ya mchakato kukamilika tulitakiwa kufuata leseni zetu kwa Meneja wa WMA wa Mkoa.

Meneja wa WMA Mkoa wa Dodoma,  Ibrahim Said ambaye aliratibu kikao kazi na mafunzo, alibainisha kuwa Ofisi yake imekuwa ikiandaa kikao kazi na wadau wa vipimo kila baada ya miezi mitatu kwa lengo la kukumbushana majukumu ya kazi pamoja na kutatua changamoto ambazo hukutana nazo majukumu ya kila siku.

“Miongoni mwa changamoto iliyokuwa inatukabili kwa sasa ni uelewa wa Mfumo mpya wa kujisajili ambao Wakala tumeanzisha hivi karibuni ambapo mafundi wetu wote wanatakiwa kuutumia kuweka zao kwa ajili ya maombi ya leseni kwa shughuli wanazofanya,” alieleza.

Alisema kuwa kutokana na changamoto hiyo, Ofisi yake iliona ni kikao kazi hicho kikaambatana na mafunzo ya namna ya kutumia mfumo huo.

Mfumo huo mpya wa kujisajili mafundi na waundaji vipimo nchini unatambulika kama OSA (Online Service Application) na unapatikana kupitia kiungo osa.wma.go.tz ukiwa ni sehemu ya Mfumo Mama wa WMA uitwao WMA-MIS.

Wakala wa Vipimo ndio wenye dhamana ya sekta ya vipimo vya kuzingatia nchini ikiwa ni pamoja na utoaji wa leseni kwa mafundi na waandaji wa vipimo vya aina mbalimbali nchini.

Comments

Popular posts from this blog

WANAFUNZI WALIOMALIZA KIDIA SEKONDARI WACHANGIA UJENZI WA KANISA SH MILLION 20

VETA YAJIPANGA KUSHIRIKINA NA TOYOTA TANZANIA KUIMARISHA MAFUNZO YA UFUNDI MAGARI

UJENZI WA BWAWA LA KUFUA UMEME LA MTO MALAGARASI , WAPIGA HATUA MPYA