MATUMAINI MAPYA KWA VIPAJI: SERIKALI YAFUNGUKA UTEKELEZAJI WA UJENZI WA VITUO VYA MICHEZO

 




Na Mwandishi wetu

Serikali imesema kuwa inaendelea na utekelezaji wa mpango wa ujenzi wa vituo vya michezo (Sports Academies) kwa kufuata kanda, ambapo kwa sasa nguvu imelekezwa Kanda ya Ziwa kabla ya kuwafikia maeneo mengine nchini likiwemo jimbo la Bumbuli.

Hayo yamebainishwa Bungeni jijini Dodoma leo February 4, 2026 na Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Hamis Mwinjuma wakati akijibu swali la Mbunge wa Bumbuli, Mhe. Eng. Ramadhani Hamza Singano.

Katika swali lake, M Singano alitaka kujua ni lini Serikali itaanzisha Kituo cha Michezo (Sports Academy) katika jimbo la Bumbuli kwa kuwa tayari kuna eneo kubwa lililotengwa kwa ajili ya viwanja vya michezo.

Akifafanua kuhusu mpango huo,  Mwinjuma amesema Serikali inatambua umuhimu wa kusogeza huduma za miundombinu ya michezo kwa wananchi kuanzia ngazi za Mikoa, Wilaya hadi Majimbo.

"Hii ni moja ya vipaumbele katika Dira ya Maendeleo ya Taifa 2050, Ilani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) ya Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2025 na Sera ya Maendeleo ya Michezo ya Mwaka 1995," alisisitiza Mhe. Mwinjuma.

Comments

Popular posts from this blog

WANAFUNZI WALIOMALIZA KIDIA SEKONDARI WACHANGIA UJENZI WA KANISA SH MILLION 20

VETA YAJIPANGA KUSHIRIKINA NA TOYOTA TANZANIA KUIMARISHA MAFUNZO YA UFUNDI MAGARI

UJENZI WA BWAWA LA KUFUA UMEME LA MTO MALAGARASI , WAPIGA HATUA MPYA