MWANASHERIA MKUU WA SERIKALI AONGOZA KLINIKI YA SHERIA BURE MNAZI MMOJA.

 




Na Mwandishi wetu


MWANASHERIA Mkuu wa Serikali, Hamza S. Johari amewaongoza Mawakili wa Serikali kutoa huduma za ushauri wa Kisheria kwa wananchi wakati wa Kliniki ya Sheria bila malipo iliyozinduliwa tarehe 16 Februari, 2026 katika Viwanja vya Mnazi Mmoja Jijini Dar es Salaam.

Johari amemuhudumia mwananchi aliyekuja kupata huduma ya ushauri wa kisheria ambapo alimsikiliza na kumuhudumia Sarah Mohamed aliyewasilisha maombi yake changamoto ya mirathi inayomkabili.

“Tumeyapokea malalamiko yako na mimi pamoja na timu tutayafanyia kazi kwa haraka ili kuleta changamoto inayokukabili ,” amesema Mwanasheria Mkuu wa Serikali.

Katika zoezi hilo la kutoa huduma kwa wananchi Mwanasheria Mkuu wa Serikali aliambatana na Naibu Waziri wa Katiba na Sheria  Zainab A. Katimba.




Timu ya Mawakili wa Serikali kutoka Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali imeipiga katika Viwanja vya Mnazi Mmoja Jijini Dar es Salaam kutoa huduma mbalimbali za malipo bila malipo kwa wananchi wa Dar es Salaam kuanzia tarehe 16 hadi 22 Februari, 2026.

Comments

Popular posts from this blog

WANAFUNZI WALIOMALIZA KIDIA SEKONDARI WACHANGIA UJENZI WA KANISA SH MILLION 20

VETA YAJIPANGA KUSHIRIKINA NA TOYOTA TANZANIA KUIMARISHA MAFUNZO YA UFUNDI MAGARI

UJENZI WA BWAWA LA KUFUA UMEME LA MTO MALAGARASI , WAPIGA HATUA MPYA