RAIS MWINYI APONGEZA WAZO LA BUNGE KUJENGA CHUO ZANZIBAR

 


Na Mwandishi wetu

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Hussein Ali Mwinyi, amesema kuwa Zanzibar inahitaji kuwa na vyuo vikuu zaidi vitakavyosaidia kutekeleza Zanzibar katika ramani ya kimataifa kama kituo muhimu cha utoaji wa mafunzo na elimu ya viwango vya juu katika fani mbalimbali.

Rais Dkt. Mwinyi ameyasema hayo leo, tarehe 18 Februari 2026, alipokutana na wajumbe wa Tume ya Utumishi ya Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, wakiongozwa na Spika wa Bunge hilo,  Mussa Azan Zungu, waliofika Ikulu, Zanzibar.



Katika mazungumzo hayo, Rais Dkt. Mwinyi ameridhishwa na wazo la Bunge la ujenzi wa Chuo cha Mafunzo ya Diplomasia na Huduma za Bunge kinachotarajiwa kujengwa Zanzibar, akieleza mradi huo ni fursa adhimu kwa taifa. Amesema kuwa uwepo wa chuo hicho utachochea ujio wa wanafunzi na kutuma ujumbe kutoka mataifa mbalimbali kuja kujifunza Zanzibar, hali itakayochangia uchumi huo kuchangia sekta ya elimu na huduma nayo.

Aidha, Rais Dkt. Mwinyi amewakabidhi wajumbe hao kuwa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ipo tayari katika utekelezaji wa mradi huo na kuwataka wajumbe wa Tume hiyo kulifanikisha hilo kwa haraka ili Zanzibar iweze kunufaika na fursa hiyo mapema.





Kwa upande wake, Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,  Mussa Azan Zungu, amempongeza Rais Dkt. Mwinyi kwa uongozi wake thabiti ulioleta mabadiliko makubwa ya maendeleo Zanzibar, hususan katika ujenzi wa ujenzi wa barabara na kasi ya ukuaji wa uchumi unaoendana na mabadiliko ya dunia.




Wajumbe wa Tume ya Utumishi wa Bunge lako Zanzibar kwa ajili ya mafunzo ya siku tatu ya uongozi kwa Kamati ya Uongozi na Tume ya Utumishi ya Bunge, iliyofanyika Tunguu, Mkoa wa Kusini, Unguja.

Comments

Popular posts from this blog

WANAFUNZI WALIOMALIZA KIDIA SEKONDARI WACHANGIA UJENZI WA KANISA SH MILLION 20

VETA YAJIPANGA KUSHIRIKINA NA TOYOTA TANZANIA KUIMARISHA MAFUNZO YA UFUNDI MAGARI

UJENZI WA BWAWA LA KUFUA UMEME LA MTO MALAGARASI , WAPIGA HATUA MPYA