RAIS WA CAF AWASILI TANZANIA





Na Mwandishi wetu

RAIS wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF), Dkt. Patrice Motsepe, amewasili nchini leo Februari 13, 2026 kwa ajili ya kuhudhuria na kuongoza mkutano wa Kamati Tendaji wa shirikisho hilo.

Dkt. Motsepe amepokelewa na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Paul Makonda, katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, Dar es Salaam.

Mkutano huo unafanyika katika Hoteli ya Hyatt Regency Dar es Salaam, The Kilimanjaro na unatarajiwa kukutanisha viongozi mbalimbali wa soka barani Afrika kujadili masuala muhimu yanayohusu maendeleo ya mpira wa miguu.




Kuwa mwenyeji wa mkutano huo ni ishara ya kuimarika kwa nafasi ya Tanzania katika ramani ya soka barani Afrika, hususan katika kipindi hiki cha maandalizi ya mashindano ya AFCON 2027.

Comments

Popular posts from this blog

WANAFUNZI WALIOMALIZA KIDIA SEKONDARI WACHANGIA UJENZI WA KANISA SH MILLION 20

VETA YAJIPANGA KUSHIRIKINA NA TOYOTA TANZANIA KUIMARISHA MAFUNZO YA UFUNDI MAGARI

UJENZI WA BWAWA LA KUFUA UMEME LA MTO MALAGARASI , WAPIGA HATUA MPYA