UMEME NI KIPAUMBELE KATIKA MAENEO YA UCHIMBAJI MADINI -DAS KAHAMA
Afungua kikao kazi kati ya TANESCO na Madiwani Halmashauri ya Wilaya ya Msalala
Aipongeza TANESCO kwa kuwashirikisha Madiwani miradi ya umeme
N Mwandishi wetu
KATIBU Tawala wa Wilaya ya Kahama, mkoani Shinyanga, Glory Muslim, amesema kuwa nishati ni muhimu na nisikilize katika maeneo ya uchimbaji madini mchango wake katika kufungua fursa za rasilimali na maendeleo ya mamlaka pamoja na wananchi kwa ujumla.
Akizungumza wakati wa kikao kazi kati ya TANESCO na madiwani kutoka kwa Wilaya ya Msalala kwa niaba ya Mkuu wa Wilaya ya Kahama, Februari 16, 2026, Katibu Tawala huyo ameipongeza TANESCO kuhusu vile wake wa kuwashirikisha madiwani maendeleo ya miradi ya umeme na kazi zinazofanywa na Shirika kwa kuwa madiwani ni wawakilishi wa wananchi katika maeneo yao, hivyo ni rahisi kupeleka taarifa kwa moja.
Aidha, amesema licha ya kazi kubwa inayoendelea na TANESCO katika kufikisha umeme kwenye maeneo ya uchimbaji, bado kuna haja ya kuhifadhi kuhifadhi kama zahanati na shule zinafikiwa na huduma hiyo muhimu.
Naye Kaimu Meneja wa TANESCO Mkoa wa Shinyanga, Antony Tarimo, amesema kuwa TANESCO imetekeleza miradi ya kimkakati, ikijumuisha upanuzi wa vituo vya kupokea na kusambaza umeme vya Bulyanhulu na Buzwagi, ili kuondoa changamoto ya upatikanaji wa umeme katika maeneo hayo.
“Mahitaji ya umeme yamekuwa yakiongezeka sambamba na kukua kwa shughuli za kiuchumi. Hata hivyo, tayari tumetekeleza miradi ya kimkakati ya upanuzi wa vituo vya kupokea na kusambaza umeme vya Bulyanhulu na Buzwagi ili kusaidia wananchi wanapata umeme wa uhakika,” alisisitiza Tarimo.
Haya yanajiri ikiwa ni muendelezo wa jitihada za TANESCO za kufanya mikutano inayowakutanisha madiwani, wenyeviti wa serikali za mitaa na watendaji wa kata, kwa lengo la kuwajengea uwezo kuhusu miradi ya umeme katika maeneo yao, watetezi wa umeme, matumizi sahihi ya umeme pamoja na matumizi ya nishati safi ya kutumia umeme.

.jpg)

Comments
Post a Comment