EWURA YAAHIDI USHIRIKIANO NA KAMPUNI ZA MAFUTA

 




Na Mwandishi Wetu 

MKURUGENZI Mkuu wa Mamlaka ya Udhibiti wa Nishati na Maji (EWURA), Dk James Mwainyekule,  amewahakikishia ushirikiano wamiliki wa Kampuni za Bidhaa za Mafuta aina ya Petroli nchini (OMCs).

Dk Mwainyekule ametoa hakikisho hilo, Machi 4, 2026 aliposhiriki kikao cha ngazi ya juu cha OMCs kilichoitishwa na Waziri wa Nishati Deogratias Ndejembi,  ili kujadili mikakati ya iliyowekwa na serikali kuimarisha hali ya upatikanaji wa mafuta hususani kipindi hiki cha migogoro inayoendelea baina ya nchi za Irani na Marekani. 

Amesema EWURA itatoa ushirikiano wa kutosha kwa kampuni hizo, ili kuhakikisha shughuli zao hazikwami, huu akisisitiza kuwa yeyote atakayekiuka utaratibu atachukuliwa hatua kwa mujibu wa sheria.

Katika kikao hicho kilichofanyika katika ofisi ndogo za Wizara ya Nishati Dar es Salaam, Waziri Ndejembi alisema serikali imejipanga vizuri kuhakikisha mafuta yanakuwepo ya kutosha.

"Napenda kuwahakikishia kuwa Serikali imechukua hatua stahiki kuhakikisha changamoto zinazotokana na mzozo wa Iran na Marekani hauleti athari kwenye mafuta na tutashirikiana na nyie kutatua," amesema. 

“Serikali iko macho, imejipanga na  imefanya kila linalowezekana kuhakikisha uhakika wa upatikanaji wa mafuta, na tutawapatia ishirikiano wa hali ya juu, ni rai yangu kwa kila mmoja kufuata sheria za nchi.” 

Aidha, aliwaomba kutoa ushirikiano wakati wote kwa kuhakikisha kuwa watanzania wanapata huduma za mafuta bila kikwazo chochote.

Comments

Popular posts from this blog

WANAFUNZI WALIOMALIZA KIDIA SEKONDARI WACHANGIA UJENZI WA KANISA SH MILLION 20

VETA YAJIPANGA KUSHIRIKINA NA TOYOTA TANZANIA KUIMARISHA MAFUNZO YA UFUNDI MAGARI

UJENZI WA BWAWA LA KUFUA UMEME LA MTO MALAGARASI , WAPIGA HATUA MPYA