EWURA YATANGAZA BEI ZA MAFUTA MACHI 4,2026

 





Na Mwandishi wetu

MAMLAKA  ya Udhibiti wa Nishati na Maji (EWURA) imetangaza bei kikomo mpya za mwezi Machi 2026. 

Katika marekebisho hayo, watumiaji wa dizeli wameathirika zaidi ikilinganishwa na wale wa petroli na mafuta ya taa. Ongezeko hilo linagusa mafuta yanayoingizwa kupitia Bandari za Dar es Salaam, Tanga na Mtwara.

Bei hizi zimepanda kutokana na ongezeko la bei za mafuta kwenye soko la dunia na gharama za usafirishaji. Mikoa yenye bei kubwa zaidi ya petroli ni Kagera (Bukoba) na Geita, ambapo petroli inafikia Sh3,114 na Sh3,064 kwa lita moja.

Jijini Dar es Salaam, bei mpya ya petroli ni Sh2,864 kwa lita moja (ongezeko la takriban Sh76 kutoka mwezi uliopita), dizeli Sh2,858 na mafuta ya taa Sh2,932, Bei hizi ni bei kikomo, hivyo vituo vya mafuta vinaweza kuuza chini kidogo lakini haziruhusiwi kuzidi.

Watumiaji wameshauriwa kuangalia bei rasmi na kudai risiti kila wanaponunua, bei hizi zinaanza kutumika mara moja na EWURA inaendelea kufuatilia ili kuhakikisha ushindani wa haki na ulinzi wa wanunuzi.

Comments

Popular posts from this blog

WANAFUNZI WALIOMALIZA KIDIA SEKONDARI WACHANGIA UJENZI WA KANISA SH MILLION 20

VETA YAJIPANGA KUSHIRIKINA NA TOYOTA TANZANIA KUIMARISHA MAFUNZO YA UFUNDI MAGARI

UJENZI WA BWAWA LA KUFUA UMEME LA MTO MALAGARASI , WAPIGA HATUA MPYA