KAMISHNA MWENDA AWASISITIZA WANAWAKE KUWA MSTARI WA MBELE KUDAI RISITI

 



Na Mwandishi wetu

WANAWAKE nchini wamehimizwa kuwa mstari wa mbele katika kudai risiti kila wanapofanya manunuzi, hatua itakayosaidia kuimarisha uwajibikaji wa wafanyabiashara pamoja na kuongeza ukusanyaji wa mapato ya serikali.

Akizungumza katika hafla maalum ya maadhimisho ya siku ya Wanawake Duniani yaliyoandaliwa na Wanawake wa TRA, Kamishna Mwenda amesema kuwa takwimu zinaonesha kuwa idadi kubwa ya wanaofanya manunuzi katika familia na jamii ni wanawake, hivyo wana nafasi muhimu ya kuhamasisha utamaduni wa kudai risiti pindi wanaponunua bidhaa au huduma.



Amesema kuwa kudai risiti ni moja ya njia muhimu ya kuhakikisha wafanyabiashara wanazingatia sheria za kodi na kuchangia ipasavyo katika maendeleo ya taifa.

Aidha, Kamishna Mwenda amewataka wanawake pia kuhamasishana kuhusu umuhimu wa kusajili biashara zao, hususan kwa wale wanaofanya biashara kupitia mitandao ya kijamii bila kuwa na usajili rasmi.

Amesisitiza kuwa ni muhimu kwa wafanyabiashara wa mtandaoni kujisajili ili kufanya shughuli zao kwa mujibu wa sheria, kulinda biashara zao na kuchangia kikamilifu katika ukuaji wa uchumi wa nchi.

Comments

Popular posts from this blog

WANAFUNZI WALIOMALIZA KIDIA SEKONDARI WACHANGIA UJENZI WA KANISA SH MILLION 20

VETA YAJIPANGA KUSHIRIKINA NA TOYOTA TANZANIA KUIMARISHA MAFUNZO YA UFUNDI MAGARI

UJENZI WA BWAWA LA KUFUA UMEME LA MTO MALAGARASI , WAPIGA HATUA MPYA