MWANASHERIA MKUU WA SERIKALI AAPISHWA KUWA KAMISHNA WA TUME YA UTUMISHI WA MAHAKAMA







Na Mwandishi wetu

MWANASHERIA Mkuu wa Serikali,  Hamza S. Johari tarehe 13 Machi, 2026 ameapishwa kuwa Kamishna wa Tume ya Utumishi wa Mahakama, katika hafla fupi ya uapisho iliyofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Tume ya Utumishi wa Mahakama, Jijini Dodoma.

Johari ameapa mbele ya Mwenyekiti wa Tume ya Utumishi wa Mahakama na Jaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania, Mhe. George M. Masaju,  kufuatia kuteuliwa kuwa Mjumbe wa Tume hiyo.

Mwanasheria Mkuu wa Serikali ameteuliwa kuwa mjumbe wa Tume ya Utumishi wa Mahakama kufuatia kuteuliwa kwake kuwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali kwa mara ya pili na Rais wa Jamhuri  ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan Novemba, 2025




Aidha, Mwanasheria Mkuu wa Serikali ameapishwa kuwa Kamishna  kutimiza  takwa la Sheria ya Usimamizi wa Mahakama Na. 4  Sura ya 237 inayomtaka kila Kamishna kuapishwa na Mwenyekiti wa Tume ya Utumishi wa Mahakama kabla ya kuanza kutekeleza majukumu yake.

Sambamba na  Johari, Wajumbe wengine wa Tume ya Utumishi wa  Mahakama walioapishwa ni pamoja na Jaji wa Mahakama ya Rufaa Gerson Mdemu, na Mawakili wa Kujitegemea Thomas Nyanduga na Dorcas Mutabuzi.

Comments

Popular posts from this blog

WANAFUNZI WALIOMALIZA KIDIA SEKONDARI WACHANGIA UJENZI WA KANISA SH MILLION 20

VETA YAJIPANGA KUSHIRIKINA NA TOYOTA TANZANIA KUIMARISHA MAFUNZO YA UFUNDI MAGARI

UJENZI WA BWAWA LA KUFUA UMEME LA MTO MALAGARASI , WAPIGA HATUA MPYA