TUNAIMARISHA AKIBA YA MAFUTA NCHINI - DKT SAMIA

 




Na Mwandishi wetu

RAIS wa Jamhuri ya Muungano  wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan amesema kutokana na baada ya uwepo wa mapigano kati ya Marekani na Israel dhidi ya Iran,  bei ya mafuta duniani imepanda kwa asilimia 13.

Ameongeza kuwa kutokana na vita hivyo kuna kila sababu kuimarisha akiba ya hifadhi ya mafuta ili Tanzania isiathirike na upandaji wa bei ya nishati hiyo.

“Kama tunavyoona misukosuko iliyotokea hapa karibuni wiki iliyopita na tunayoendelea nayo, tayari imeshapandisha bei ya mafuta kwa 13% hadi jana, sasa hatujui leo na siku zijazo lakini tumuombe Mungu watu wale wakae juu ya meza wazungumze wakubaliane na misukosuko hii iishe ili dunia irudi katika hali ya kawaida kuendesha chumi za nchi zetu," amesema

Rais Samia amesema hayo baada ya kuweka jiwe la msingi la mradi wa ujenzi wa Matanki ya kupokea mafuta katika Bandari ya Dar es salaam katika eneo la Kigamboni Jijini Dar es salaam, leo March 03, 2026.

Comments

Popular posts from this blog

WANAFUNZI WALIOMALIZA KIDIA SEKONDARI WACHANGIA UJENZI WA KANISA SH MILLION 20

VETA YAJIPANGA KUSHIRIKINA NA TOYOTA TANZANIA KUIMARISHA MAFUNZO YA UFUNDI MAGARI

UJENZI WA BWAWA LA KUFUA UMEME LA MTO MALAGARASI , WAPIGA HATUA MPYA