WADAU WATAKIWA KUUNGA MKONO MALEZI YA WATOTO WENYE MAHITAJI MAALUM.
Na Jackline Minja, WMJJWM
MBEYA
NAIBU Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Mhe. Mhandisi Maryprisca Mahundi, amewataka wadau mbalimbali mkoani Mbeya, na kituo cha kulea watoto wenye usonji cha Funguka Foundation kilichopo Kata ya Ilomba, ili kusaidia juhudi za malezi na huduma kwa watoto wenye mahitaji maalum.
Mahundi ametoa wito huo alipofanya ziara katika kituo hicho Machi 07, 2026.
Amesema kazi ya kulea na kuwahudumia watoto wenye mahitaji maalum ni jukumu la pamoja la jamii, hivyo kuna umuhimu wa wadau mbalimbali kujitokeza kusaidia vituo vinavyotoa huduma hizo.
Kazi inayofanywa hapa ni kubwa na umuhimu kwa kuwa inahusisha kuwalea na kuwahudumia watoto wenye mahitaji maalum. Tunapaswa kumuunga mkono meneja wa kituo hiki ili awe na nguvu zaidi ya kuendelea kutoa huduma bora kwa watoto hawa,” amesema Mahundi.
Amesema watu wanaojitoa kuwahudumia watoto wanaotoa mchango mkubwa kwa jamii na taifa kwa ujumla, hivyo wanastahili kuungwa mkono na kuthaminiwa.
“Nitahakikisha suala la watoto wenye mahitaji maalum linaendelea kutoa fursa ili waweze kupata huduma stahiki.
"Nawapongeza sana wale wanaojitoa kuwahudumia watoto hawa kwani wanatoa mchango mkubwa kwa jamii na Taifa." Amesema Nassir Ally.
Naye Meneja wa kituo cha Funguka Foundation Nelly Elisha ameishukuru Serikali kupitia Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum kwa kuendelea kukisaidia kituo hicho kwa mahitaji muhimu na kuwafikisha wadau wanao maendeleo ya kituo hicho.
Aidha, mmoja wa wazazi wa watoto wanaolelewa katika kituo hicho, Bi. Zulfa Abdul Lyimo ameipongeza Serikali kwa juhudi zake za kuwajali watoto wenye mahitaji maalum na kuahidi kuendelea na kituo hicho ili kusaidia kupata malezi bora na fursa za maendeleo.



Comments
Post a Comment