WANAWAKE TFS WAGUSA MIOYO YA WAGONJWA MADABA







-๐™’๐™–๐™ฉ๐™ค๐™– ๐™ข๐™ž๐™จ๐™–๐™–๐™™๐™– ๐™ซ๐™ž๐™ฉ๐™ช๐™ค ๐™ซ๐™ฎ๐™– ๐™–๐™– ๐™ ๐™ช๐™š๐™ก๐™š๐™ ๐™š๐™– ๐™Ž๐™ž๐™ ๐™ช ๐™ฎ๐™– ๐™’๐™–๐™ฃ๐™–๐™ฌ๐™–๐™ ๐™š ๐˜ฟ๐™ช๐™ฃ๐™ž๐™–๐™ฃ๐™ž


Na Mwandishi Wetu,MADABA, RUVUMA. 

WAKALA wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS), kupitia Shamba la Miti Wino kwa sehemu ya Halmashauri ya Wilaya ya Madaba, wametoa msaada muhimu kwa wagonjwa na wasiojiweza katika vituo vya afya vya Mtyangimbole na Madaba, ikiwa ni maandalizi ya maandalizi ya Siku ya Wanawake Duniani.

Msaada huo umetolewa na watumishi wanawake wa TFS katika zoezi lililolenga kugusa maisha ya watu wenye uhitaji huku likionesha mshikamano wa kijamii kwa vitendo.

Akizungumza wakati wa kukabidhi msaada huo kwa niaba ya Mhifadhi Mkuu wa Shamba la Miti Wino mapema Wiki hii, Mhifadhi Martha Ndyetabula alisema hatua hiyo inalenga kuwafikia wagonjwa na wasiojiweza ili nao wajione kuwa ni sehemu ya utekelezaji wa siku hiyo muhimu kimataifa.





Alisema wanawake wana nafasi kubwa katika kuleta faraja na imani kwa jamii, hivyo ni muhimu kutekeleza ahadi hiyo kuonesha upendo, huruma na mshikamano kwa vitendo

"Kama wanawake tunapaswa kutumia nafasi hii kuonesha upendo na mshikamano kwa wengine. Maadhimisho haya yana maana zaidi pale yanapogeuzwa kuwa matendo halisi yanayogusa maisha ya watu wenye uhitaji," alisema Ndyetabula.

Ali kuwa TFS itaendelea na jamii katika shughuli mbalimbali zinazosaidia kuboresha ustawi wa wananchi na kuboresha mahusiano kati ya taasisi na jamii zunguka katika shughuli zake.





Kwa upande wao, baadhi ya wagonjwa na wananchi waliopokea msaada huo walishukuru TFS na Halmashauri ya Madaba kwa kuwajali watu wenye uhitaji, wakisema msaada huo umewapa faraja na kuomba msaada wakati wa matibabu.


Siku ya Wanawake Duniani huadhimishwa kila mwaka tarehe Machi, ikiwa ni jukwaa la mchango wa wanawake katika maendeleo ya jamii na kusisitiza usawa wa kijinsia.

Kwa mwaka huu, maagizo hayo yanaongozwa na kaulimbiu isemayo: “Haki kwa Wanawake na Wasichana: Msingi Jumaishi wa Kufikia Dira ya 2050.”

Comments

Popular posts from this blog

WANAFUNZI WALIOMALIZA KIDIA SEKONDARI WACHANGIA UJENZI WA KANISA SH MILLION 20

VETA YAJIPANGA KUSHIRIKINA NA TOYOTA TANZANIA KUIMARISHA MAFUNZO YA UFUNDI MAGARI

UJENZI WA BWAWA LA KUFUA UMEME LA MTO MALAGARASI , WAPIGA HATUA MPYA