WANAWAKE TTCL WASHEHEREKEA SIKU YA WANAWAKE NA WATOTO JKCI





Na Mwandishi Wetu

WANAWAKE  wa Shirika la Mawasiliano Tanzania ( TTCL) wameungana na Wanawake wengine   kuadhimisha siku ya wanawake duniani kwa kutoa msaada wa vifaa mbalimbali kwa watoto wenye matatizo ya moyo waliolazwa Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete ( JKCI) kama ishara ya faraja kwao

Akizungumza kwa niaba  ya wanawake zaidi ya 400 wa Shirika hilo leo Ofisa Uhusiano TTCL Adeline Berchimance amesema msaada huo ni  utaratibu wa kawaida wa shirika katika kujali kazi na utu

" Kama tunavyofahanu kuwa kiongozi wetu wa nchi anahamasisha kufanya kazi kwa kujali utu wanawake wa TTCL tumeamua kumuunga mkono rais wetu Dkt Samia Suluhu katika usemi wake wa Kazi na Utu," ameswma Berchimance

Ameongeza kuwa TTCL katika kuadhimisha siku ya wanawake duniani kwa mwaka 2026 wameweza kuchangishana na kununua vifaa  mbalimbali kwa ajili ya watoto na wazazi waliolazwa JKCI



Aidha Berchimance amevitaja vifaa vilivyokabidhiwa JKCI kuwa ni pamoja na Pampers,maziwa na taulo za kike ambazo zitawasaidia watoto, wazazi na walezi  hospitalini hapo

Pia amewapongeza wauguzi na madaktari kwa kusimamia taaluma zao kwa kutoa msaada wa matibabu kwa kuzingatia utaratibu huku akiahidi  kuwa wanawake wa TTCL wataendelea kujitoa kwa hali na mali katika kulinda na kuwafariji wagonjwa wa JKCI



Kwa upande wake Mkurugenzi wa Tiba Shirikishi na Daktari Bingwa Mbobezi magonjwa ya moyo kwa watoto na Daktari Bingwa Mbobezi magonjwa ya moyo kwa watoto  Dkt. Naizihijwa Majani  akiongea kwa niaba ya Mkurugenzi amesema tatizo la moyo kwa watoto lipo na JKCI imekuwa ikitoa tiba sahihi

"Kati ya watoto  100 wanaozaliwa nchini  mmoja au wawili wanagundulika kuwa na tatizo la moyo na kwamba ugonjwa huo upo katika makundi mawili," amesema Dkt.Majani

Amesema  katika watoto  milioni 2 wanaozaliwa nchini  kwa mwaka 16,000 wanakutwa na tatizo la moyo ambapo JKCI imekuwa ikiwahudumia kwa ufasaha ili kuokoa maisha yao

Dkt.Majani amezitaja dalili za magonjwa ya moyo kwa watoto kuwa ni pamoja na kutokukua vizuri, kuhema harakaharaka, kushindwa kunyonya, uzito kupungua, kukohoa mara Kwa mara, kuumwa kifua na utapiamlo

Amezitaja dalili zingine kuwa ni kifua kupanuka moyo kwenda mbio, kushindwa kucheza na wenzake, kushindwa au kuchelewa kutembea,  kuchuchumaa mara kwa mara na kuchoka bila sababu

Amewaasa wazazi walezi na watanzania kwa ujumla wanapoona dalili hizi kwa watoto kuwapeleka hospitali kwa ajili ya kufanyiwa uchunguzi



Comments

Popular posts from this blog

WANAFUNZI WALIOMALIZA KIDIA SEKONDARI WACHANGIA UJENZI WA KANISA SH MILLION 20

VETA YAJIPANGA KUSHIRIKINA NA TOYOTA TANZANIA KUIMARISHA MAFUNZO YA UFUNDI MAGARI

UJENZI WA BWAWA LA KUFUA UMEME LA MTO MALAGARASI , WAPIGA HATUA MPYA