ABDILATIF ABDALLAH KUWA MGENI RASMI TUZO ZA MWALIMU NYERERE 2026
Na Mwandishi wetu
MSHAIRI Maarufu Duniani Abdilatif Abdalah kutoka nchini Ujerumani anatarajiwa kuwa Mgeni Rasmi katika hafla ya Nne ya Tuzo ya Taifa ya Mwalimu Nyerere ya Uandishi Bunifu mwaka 2026.
Akizungumza na Waandishi wa Habari Aprili 8, 2026 Jijini Dodoma, Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Adolf Mkenda amesema kuwa Abdilatif Abdallah ana asili ya Afrika Mashariki na si mgeni kwa Tanzania kwani aliwahi kuishi na kufundisha katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kwa zaidi ya miaka 15.
"ujio wake ni heshima kubwa kwa Tanzania na mchango wake katika kukuza kazi za uandishi bunifu utakuwa na manufaa kwa mataifa ya Afrika Mashariki," aliongeza Prof Mkenda.
Aidha, ameongeza kuwa kabla ya hafla ya utoaji tuzo kutakuwa na mjadala wa wadau walioshirikisha wasanii maarufu Tanzania pamoja na wageni mashuhuri ambao ni Dkt. Aida Mutenyo kutoka Uganda na Ferdinand Ndahayo kutoka Rwanda.





Comments
Post a Comment