BODI YA WAKURUGENZI EDTCO YARIDHISHWA NA KASI YA MRADI TABORA–KIGOMA
Na Mwandishi wetu
BODI ya Wakurugenzi wa Kampuni ya Ujenzi na Ukarabati wa Miundombinu ya Usafirishaji na Usambazaji wa Umeme (ETDCO) imeonyesha kuridhishwa na utekelezaji wa miradi ya umeme kutoka Mkoa wa Tabora hadi Kigoma na kuwahimiza wananchi kuchangamkia fursa za uwepo wa nishati hiyo.
Hayo yamebainishwa na Mwenyekiti wa bodi hiyo, Raymond Mbilinyi, wakati akizungumza na waandishi wa habari Mkoani Kigoma katika ziara yao ya kukagua miradi mbalimbali inayotekelezwa na ETDCO.
"Katika miradi yote tuliyoitembelea kuanzia Tabora mpaka Kigoma, tumekuta utekelezaji wake unakwenda vizuri. Ningependa kuwapongeza menejimenti ya ETDCO na wafanyakazi wote kwa kuhakikisha utekelezaji wa miradi unafanyika kama ilivyopangwa," amesema Mha. Mbilinyi.
Kwa upande wao, wajumbe wa bodi hiyo Adv. Florida Mapunda na CPA Richard Manamba wamefurahishwa na ziara hiyo iliyowawezesha kujionea miradi ya umeme





Comments
Post a Comment