KATIBU MKUU CCM AKUTANA NA MJUMBE MAALUM WA JUMUIYA YA MADOLA

 




Na Mwandishi wetu 

KATIBU Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Asha-Rose Migiro, leo tarehe 15 Aprili 2026 amefanya mazungumzo na Mjumbe Maalum wa Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Madola na Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Malawi, Mhe. Lazarus Chakwera, katika Ofisi za CCM Lumumba, jijini Dar es Salaam.

Mazungumzo hayo yalijikita katika hali ya kisiasa nchini pamoja na matukio ya wakati na baada ya Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 2025.

Chakwera yupo nchini Tanzania kwa ziara maalum katika nafasi yake kama Mjumbe Maalum wa Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Madola, Mhe. Shirley Ayorkor Botchwey. 




Kikao hicho ni sehemu ya mashauriano yake na wadau mbalimbali wa kitaifa kwa lengo la kubadilishana mawazo kuhusu maendeleo ya kisiasa baada ya Uchaguzi Mkuu wa tarehe 29 Oktoba 2025, pamoja na juhudi zinazoendelea za kuimarisha amani, demokrasia na mshikamano wa kitaifa nchini Tanzania.




Comments

Popular posts from this blog

WANAFUNZI WALIOMALIZA KIDIA SEKONDARI WACHANGIA UJENZI WA KANISA SH MILLION 20

VETA YAJIPANGA KUSHIRIKINA NA TOYOTA TANZANIA KUIMARISHA MAFUNZO YA UFUNDI MAGARI

UJENZI WA BWAWA LA KUFUA UMEME LA MTO MALAGARASI , WAPIGA HATUA MPYA