MASHINDANO YA DUNIA YA KUHIFADHI QURAAN KUFANYIKA KWA MKAPA APRIL 5

 




Na Mwandishi wetu

MAKAMU wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Hemmed  Suleiman Abdulla anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika  nufusu fainali ya Mashindano ya Dunia ya Kuhifadhi Quraan Tukufu kwa washiriki wa ndani.

Akizungumza na waandishi wa habari  Dar es Salaam, Mwenyekiti wa Jumuiya ya Kuhifadhisha  Quraan Tanzaniam, Sheikh Othuman Kapolo, amesema nusu fainali hiyo itafanyika  Aprili 2 mwaka huu katika  Hoteli ya Golden Tulip Uwanja wa Ndege,  Unguja, Zanzibar.

Sheikh  Kapolo amesema nusu fainali hiyo  ni kuele fainali ya mashindano hayo itakayofanyika Aprili 5mwaka huu katika Uwanja wa Benjamin Mkapa.

"Tayali  washiriki wa fainali hiyo  kutoka mataifa mbalimbali  duniani wameanza kuwasili nchini.Hadi kufikia Ijumaa wiki hii tunatarajia tutakuwa tumepokea washiriki wote 26 kutoka mataifa mbalimbali duniani yaliyothibitishwa kushiriki,"ameeleza Shekh Kapolo.

Amesema jumla ya zawadi zote kwa washindi ni sh. milioni 125 ambapo pia kutakuwa na zawadi kwa wananchi watakaofika katika Uwanja wa Benjamin Mkapa Aprili 25  kushuhudia fainali hiyo, ambazo ni pamoja na simu za mkononi, pikipiki, pikipiki za mizigo 'Guta' na tiketi za umra.

Awali, akizungumza kwa niaba ya Mwakilishi wa Mufti na Sheikh Mkuu wa Tanzania, Dk. Aboubakar Zuberi, Sheikh Hassan  Chizenga, amesema   mashindano hayo ya Dunia ya Kuhifadhi Quraan yamekuwa alama ya kuitambulisha Tanzania kitaifa na  kimataifa hivyo kuwataka wananchi wote bila kujali itikadi zao za kidini  kushuhudia.

Comments

Popular posts from this blog

WANAFUNZI WALIOMALIZA KIDIA SEKONDARI WACHANGIA UJENZI WA KANISA SH MILLION 20

VETA YAJIPANGA KUSHIRIKINA NA TOYOTA TANZANIA KUIMARISHA MAFUNZO YA UFUNDI MAGARI

UJENZI WA BWAWA LA KUFUA UMEME LA MTO MALAGARASI , WAPIGA HATUA MPYA