DAS KIGAMBONI AZINDUA OFISI YA WILAYA YA KITANESCO YA KIMBIJI
Asema itapunguza adha ya safari ya safari ndefu kufuata huduma
Aipongeza TANESCO kwa maboresho yanayoendelea kwa wateja wake
KATIBU Tawala Wilaya ya Kigamboni Upendo Mahalu amezindua Ofisi mpya ya Wilaya ya KiTANESCO Kimbiji ikiwa ni mkakati wa Shirika wa kuendelea kuwahudumia karibu na kusogeza huduma na wananchi.
Akizugumza Mei 04, 2026 kwa niaba ya Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni, Katibu Tawala wa Wilaya hiyo, Bi. Upendo Mahalu, amesema Ofisi hiyo umelenga kuboresha kwa wananchi mahitaji mahitaji ya umeme yanavyozidi kuongezeka.
Ameeleza kuwa hatua hiyo inaakisi maboresho ya kiutendaji yanayolenga kuongeza ufanisi na gharama ya umbali kwa wananchi ambao hapo awali walilazimika kufuata huduma katika ofisi za mkoa zilizopo Tungi Mnadani.
“Lengo la kuboresha huduma kwa wananchi na kasi ya kuboresha huduma kwa wananchi na kasi ya kusaidia la mahitaji ya umeme kwa maendeleo ya nchi. Naipongeza Menejimenti ya TANESCO kwa maono ya kusogeza huduma karibu na wananchi,” alisisitiza Bi. Mahalu.
Kwa upande wake, Mbunge wa Jimbo la Kigamboni, Haran Sanga, ameipongeza TANESCO kwa maboresho makubwa ya kiutendaji na kimtazamo, hukutaka wananchi kuwa mstari wa mbele akiwa kulinda umeme, akisisitiza kuwa serikali inawekeza fedha nyingi katika sekta hiyo.
Akizungumza Kaimu Meneja Huduma kwa Wateja, Shamu Lameck, amesema TANESCO inaendelea huduma zake kwa wateja kwa kutoa elimu na taarifa sahihi kuhusu matumizi ya umeme na mawasiliano yake.
Ofisi ya TANESCO Kimbiji itahudumia kata za Kimbiji, Somangila, Pembamnazi na Kisarawe II. Uzinduzi huo pia uliambatana na kukabidhiwa kwa vitendea kazi, yakiwemo magari na bajaji yatakayosaidia kuwafikia wateja kwa haraka na kwa ufanisi zaidi.






Comments
Post a Comment