MAJALIWA- UWEKEZAJI KATIKA HISA UJENGA MUSTAKABALI WA KIFEDHA

 




Na Mwandishi wetu

WAZIRI Mkuu Mstaafu na Mshauri wa Rais ,Kassim Majaliwa amesema uwekezaji katika hisa ni njia salama ya kujenga mustakabali wa kifedha  Kwa mtu binafsi na Taifa.

Akizungumza katika hafla ya uzinduzi huo Jijini Dar es salaam mapema leo Mei ,2026 Majaliwa amesema mafanikio ya MCB ni ushahidi wa maono mazuri ya walimu walioanzisha benki hiyo, ambayo sasa imekua kwa kasi na kutoa huduma kwa Watanzania wa kada zote bila ubaguzi.

Amesema ukuaji wa benki hiyo umejengwa juu ya misingi ya weledi, uadilifu na uaminifu wa watendaji wake, hali iliyochangia kuleta mabadiliko makubwa katika sekta ya fedha nchini.

“Leo hii tunashuhudia ndoto ya walimu ikigeuka kuwa taasisi imara kifedha. Hii ni benki inayotoa huduma kwa kila Mtanzania, si walimu pekee,” amesema 





Amesisitiza kuwa uwekezaji kwenye hisa ni njia salama na yenye manufaa ya muda mrefu, huku akiwahimiza Watanzania kuchangamkia fursa hiyo ili kujenga mustakabali wa kifedha kwa familia na taifa kwa ujumla.

Amesema kuwa kuimarika kwa mtaji wa benki hiyo kutaiwezesha kupanua utoaji wa mikopo nafuu kwa walimu, wafanyakazi, wafanyabiashara na makundi mengine ya kijamii, pamoja na kuwekeza zaidi katika teknolojia za kidijitali ili kuongeza ujumuishaji wa kifedha hadi maeneo ya vijijini.

Amebainisha kuwa mafanikio ya benki nyingi za ndani yanaonyesha uwezo wa Watanzania kusimamia taasisi za kifedha kwa ufanisi, tofauti na ilivyokuwa hapo awali ambapo uongozi wa juu ulikuwa ukitoka nje ya nchi.

“Leo benki zetu zinasimamiwa na Watanzania wenye ujuzi na matokeo yanaonekana kupitia faida na ukuaji unaoendelea,” ameongeza 





Amesema katika hatua hiyo mpya ya uwekezaji, wanahisa waliopo wamepewa fursa ya kuongeza hisa zao hadi mara tatu, huku milango ikifunguliwa pia kwa wawekezaji wapya, wakiwemo watu binafsi na taasisi mbalimbali.

Aidha amewataka viongozi na watendaji wa MCB kuendelea kubuni bidhaa mpya za kifedha na kuimarisha huduma ili kukidhi mahitaji ya wateja na kuongeza ushindani sokoni.

Kwa upande wake Ofisa Mtendaji Mkuu wa Mwalimu Commercial Bank, Richard Makungwa amesema dirisha la ununuzi wa hisa stahiki  limefunguliwa rasmi Mei  6,2026 hadi Juni 05, 2026  ambapo Wanahisa wataweza kununua hisa za benki kidigitali kupitia Application ya DSE Hisa Kiganjani ,Ofisi za Chama cha Walimu (CWT) na  matawi na ofisi za benki ya Mwalimu.

Amesema hatua hiyo mpya ni ya ukuaji wa mtaji, bali ni uthibitisho wa imani yao na dhamira ya kuendelea kujenga taasisi ya kifedha imara, endelevu na bunifu.

"Ufanisi wa miaka mitano Iliyopita katika kipindi cha miaka mitano iliyopita, Mwalimu Commercial Bank Plc. imepiga hatua kubwa za maendeleo mizania ya Benki tumeshuhudia ongezeko la jumla ya mali kutoka chini ya TZS 30 bilioni (2019) hadi TZS 98 bilioni (2025), ukuaji unaoakisi ufanisi wa usimamizi wa rasilimali na kuongezeka kwa shughuli za kibenki "amesema 



Vilevile amesema mikopo imeongezeka kutoka sh Bilioni kwa mwaka 2019 hadi sh Bilioni 66 kwa mwaka 2025 huku wakilenga wateja binafsi hususani walimu, watumishi wengine, wafanya biashara wadogo na kati (SME) ambao ni nguzo za uchumi wa Taifa.

Kwa upande wa Faida kabla ya kodi alisema imeongezeka kutoka hasara ya TZS 4.8 bilioni (2019) hadi faida ya TZS 487 milioni (2025), ikiashiria mwenendo chanya wa kibiashara na usimamizi bora wa gharama.

Aidha alisema MCB imewekeza kwa kiwango endelevu katika utoaji huduma za kidigitali ili kuongeza urahisi, usalama, na ufanisi kwa wateja wetu ambao kwa sasa wanaweza kufanya miamala kupitia simu za mkononi.

Pia alisema wateja wameongezeka kufikia zaidi ya  sh 67,000 katika kipindi cha miaka mitano. 

"Hii ni matokeo ya ubunifu wa bidhaa na huduma rafiki kwa wateja ambao ni wafanyakazi, wafanyabiashara wadogo na wa kati, taasisi, vijana na makundi maalum ya kijamii"alisema 

Naye Mwenyekiti wa Bodi ya MCB BANK, Franisis Ramadhani alisema hisa Stahiki ni fursa ya kipekee kwa wanahisa wa benki kununua hisa za ziada kwa bei ya punguzo kabla zoezi kufungwa. 

"Hatua hii ni muhimu sana kwani inalenga kuimarisha mtaji wa benki, kuwezesha ukuaji endelevu wa biashara na kuboresha huduma tunazotoa kwa wateja wetu kote nchini."alisema 

Alisema Zoezi hilo limepata idhini kutoka Benki Kuu (BOT) na litafanyika kwa  uwazi chini ya usimamizi wa Mamlaka ya Usimamizi wa Masoko na Mitaji (CMSA) na Soko la Hisa la Dar es Salaam (DSE)  kwa ushirikiano na iTrust Finance Limited ambao ni washauri 



Comments

Popular posts from this blog

WANAFUNZI WALIOMALIZA KIDIA SEKONDARI WACHANGIA UJENZI WA KANISA SH MILLION 20

VETA YAJIPANGA KUSHIRIKINA NA TOYOTA TANZANIA KUIMARISHA MAFUNZO YA UFUNDI MAGARI

UJENZI WA BWAWA LA KUFUA UMEME LA MTO MALAGARASI , WAPIGA HATUA MPYA